In Summary
  • Bila kutaja majina pia aliwaita baadhi wasanii kwa kubadilisha mazingira ya shindano hilo kuwa kiungo cha burudani.
Mchekeshaji 2mbili na mwanamuziki Ngesh.
Image: INSTAGRAM

Mtayarishaji maudhui na mwanablogu 2mbili amewasuta watu mashuhuri wa Kenya kwa mienendo yao wakati wa kukusanyika kwa mpishi wa Kenya Maliha.

Huku akimpongeza Chef Maliha kwa kuvunja rekodi hiyo 2mbili alieleza kutoridhishwa kwake na watu mashuhuri ambao kutokana na wadhifa wake walikuja kutengeneza maudhui badala ya kumuunga mkono mpishi huyo.

"Hongera mpishi Mahila kwa rekodi iliyovunjwa" aliandika akifichua kuwa baadhi ya watu mashuhuri walitangulia kujiwekea chakula ambacho kilikusudiwa kutolewa kwa watoto wa mitaani baada ya mashindano hayo.

"Kwa bahati mbaya hakutakuwa na kitu cha kuchangia watoto wa mitaani kama ilivyopangwa mapema kwa sababu watu mashuhuri walikuja na kula chakula chote (kwa maudhui)" Aliandika kwenye hadithi zake za Instagram.

Wengine walibeba hadi nyumbani kwao kwa jina la tumekuja kuku support” 2mbili aliongeza.

Bila kutaja majina pia aliwaita baadhi wasanii kwa kubadilisha mazingira ya shindano hilo kuwa kiungo cha burudani.

”It was more of an artist get together than supporting mpishi, mwingine naskia karibu aigeuze album launch gig ,acha nainze yangu ya kulala nione kama watani support.”

Mpishi Mahila ambaye sasa ndiye aliyeshikilia rekodi mpya ya dunia ya masaa marefu zaidi za kupikia jikoni za nyumbani alizopokea kwa kupika kwa saa 95 bila kukoma alipokea jumbe za pongezi kutoka kwa wasanii na watu mashuhuri.

 

 

 

 

View Comments