In Summary

•Picha iliyochapishwa na DianaJumapili ilizua mjadala mkubwa zaidi kwani gauni la kutatanisha alilokuwa amevaa lilionekana vizuri

•Wengi wa wale waliotoa maoni walionekana kumshambulia Diana kwa chaguo lake la mavazi huku baadhi wakimdhihaki.

Familia ya Bahati
Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Mtindo wa mavazi wa mwanavlogu Diana Marua wakati wa kipindi cha picha za familia umezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Wiki iliyopita, rapa huyo na mumewe Bahati walichapisha picha nzuri za familia yao kwenye kurasa zao za Instagram katika siku tofauti. Katika picha hizo, wanandoa hao na watoto wao watatu, ukiondoa mdogo wao Malkia Bahati ambaye hakuwepo, walikuwa wamevalia nguo nyeusi na nyeupe.

Picha iliyochapishwa na Diana siku ya Jumapili hata hivyo ilizua mjadala mkubwa zaidi kwani gauni la kutatanisha alilokuwa amevaa lilionekana vizuri. Mama huyu wa watoto watatu alionyesha picha yake na mtoto wao wa kulea, Morgan Bahati. Alichukua fursa hiyo kumsherehekea mvulana huyo wa miaka 13 na kukiri anampenda sana.

“Yule aliyeniita MUMMY kwanza. Baaaabbyyy wangu @morgan_bahati ni mzima. Malengo ya Mama na Mwana. Nakupenda Morgan,” Diana alisema Jumapili.

Walakini, wanamitandao wengi hawakuonekana kuyaangazia macho maneno mazuri ambayo mke huyo wa Bahati alimwandikia mwanawe Morgan bali waliangazia mavazi aliyovaa. Wengi wa wale waliotoa maoni walionekana kumshambulia kwa chaguo lake la mavazi huku baadhi wakimdhihaki.

Kundi la watumiaji wa mitandao ya kijamii waliotoa maoni yao walionekana kumshauri mama huyo wa watoto watatu kuwa makini na mavazi anayovaa mbele ya watoto wake, wengine walimkosoa, baadhi wakamtetea huku wengine wakidai kuwa suruali yake ya ndani ilionekana pichani.

Tazama baadhi ya maoni ya wanamitandao Wakenya:-

@escob3r:  Advise...... No hard feelings but truth be told you are are great mother but the dress code should change...... But kudos to your progress and keep being the good mother you are.

@evesheryk:  this is wrong...it is good for u bt embarrassing the boy to his peers .He cnt be proud to show such a pic to his peers coz her moms panty is visible.I am ua big fan n happy for ua wins bt hii sitakimya

@chelangat.bridgid: Diana b pliz wear clothes decent clothes for once.

Awour.00: your son is now grown.. wear decent clothes..ukweli nayo tutakua coz tunakupenda

i_am_njeri_whit: Can't you dress/ wear decently Infront of your kids

winfaithfulofficial: Siungevaa kitenge hata jamani mngetokea supuu Sana Infront of a teenager son

View Comments