In Summary

•Bahati alionekana akiimba huku baadhi ya mashabiki wanawake wakijitokeza jukwaani mmoja baada ya mwingine na kujumuika naye katika kunengua mauno.

•Baadhi ya mashabiki walitania kitendo hicho huku wengine wakionekana kumtagi mkewe Diana Marua na kumuonya.

Bahati akitumbuiza mjini Narok.
Image: INSTAGRAM// BAHATI

Wikendi iliyopita, mwimbaji mashuhuri wa Kenya Kelvin Kioko almaarufu Bahati alikuwa mjini Narok  ambapo alifanya shoo katika Narok Club Arena.

Kwa mujibu wa video alizoshiriki, shoo hiyo ilikuwa ya kusisimua na mashabiki waliungana naye katika kuimba ili kuifanya iwe changamfu zaidi.

Katika moja ya video hizo, mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 30 alionekana akiimba huku baadhi ya mashabiki wa kike wakijitokeza jukwaani mmoja baada ya mwingine na kujumuika naye katika kunengua mauno, kitu ambacho ameonekana kulalamikia kwa utani akidai kuwa yeye bado ni mtoto mdogo.

“Akii mimi ni mtoto mdogo wacheni kuniharibu.. mnanikosea,” Bahati alisema chini ya video aliyochapisha kwenye mtandao wa Instagram.

Katika video hiyo, Bahati alionekana akicheza wimbo wake wa ‘Mi Amor’ huku mashabiki ndani ya kilabu wakijumuika katika kuimba na kucheza densi kwa msisimko mkubwa.

Wakati akiendelea kuimba, baadhi ya mashabiki wanawake walijumuika naye jukwaani na kumtingishia kiuno, jambo ambalo alionekana kulifurahia.

“Ile kitu wewe unado, unanilose. Nitakwenda wapi. Kamoyo kangu unanido, unaniconfuse, wewe wanani?.. Nikudekeze, lalia kifuani, usiogope Diana Ma,” Bahati aliimba kabla ya kusimamisha muziki kwa muda.

Video aliyochapisha mwimbaji huyo wa zamani wa nyimbo za injili imezua hisia tofauti kutoka kwa wanamitandao wakiwemo mastaa wenzake.

Baadhi ya mashabiki walionekana kupongeza maumbile ya wanadada waliokuwa wakicheza densi na Bahati, baadhi walitania kitendo hicho huku wengine wakifanya zaidi kumtagi mkewe Diana Marua na kumuonya.

Tazama maoni ya baadhi ya wanamitandao;

mrseedofficial:Lakini unakuanga na nguvu ya kupost vitu zamaajabu 😂

vancekims:Diana come and see

githeu88:Aki si watavunjika migongo wakijaribu kuimpresss😂

jemutai.diana:Auntie madoo typing in English,,, deleting in kiswahili 😂😂😂

tumesiimedavid33:  Mama Baha where are you?😂😂😂😂😂😂the man is going

dufladilligon:Wewe sasa mpaka uwache!!! Shemeji@diana_maruahii ni mambo gani?!!!!!!!

ma_dhiba: Najua hapo Deee alisema malizana na show then tutarudia haya badayee 😂😂😂

View Comments