In Summary

•Akothee amewasihi Wakenya kuwa na utu na kukoma kuwahusisha watoto wa Bahati na Diana katika vita vyao dhidi ya wanandoa hao.

•Akothee alibainisha kuwa kitendo hicho hakiwaathiri tu Bahati na Diana bali kinaweza kuwa na athari mbaya kwa watoto wao.

Akothee amekerwa na shambulio dhidi ya familia ya Bahati.
Image: INSTAGRAM//

Mwimbaji na mjasiriamali mashuhuri Esther Akoth almaarufu Akothee ametoa tamko lake kuhusu shambulio linaloendelea dhidi ya familia ya Bahati.

Katika taarifa ndefu siku ya Jumanne, Akothee ambaye alionekana kukerwa sana na suala hilo aliwasihi wanamitandao Wakenya kuwa na utu na kukoma kuwahusisha watoto wa Bahati na Diana Marua katika vita vyao dhidi ya wanandoa hao.

Mwanamuziki huyo alishangaa kwa nini wanamitandao wanapata ujasiri wa kuwafananisha watoto wa wanandoa hao na watu wengine mashuhuri akitaja kuwa kitendo hicho kinawachora wanawake kama watu wabaya katika jamii.

“HII PHOTOHOP INATAKIWA KUISHIA HAPO KWA AJILI YA WATOTO. Ukiwachukia Bahati na Diana, Watoto wao hawana uhusiano wowote. Natamani sote tungekuwa na utu,” Akothee alisema kwenye Instagram

Aliongeza, “Mitandao ya kijamii inazidi kuwa ya kishetani. Watu wamepoteza huruma, heshima na nidhamu binafsi. Unawezaje kuchukua picha ya familia nzima na kuanza kulinganisha watoto wa watu na watu wengine? Ni nini hasa kilichokuja akilini mwako? Hiyo ni nini ilitokea? Hivi ndivyo jamii inavyowachora wanawake katika jamii hii ya kibaguzi. Itakuwa uchungu kiasi gani ikiwa ungekuwa wewe kwenye picha hii, iwe mwanamume au mwanamke, baba au mama hata watoto kwenye picha?"

Mama huyo wa watoto watano alibainisha kuwa kitendo hicho hakiwaathiri tu Bahati na Diana bali kinaweza kuwa na athari mbaya kwa watoto wao.

Aidha, alisema kuwa watu mashuhuri mara nyingi huposti picha za watoto wao kwa nia nzuri ya kutambua familia, kuhamasisha wazazi wengine na kwa burudani.

"Usichukulie jambo hili kawaida, wivu wako hautazuia watu mashuhuri kusherehekewa, ambapo Watoto wanahusika, sitamyamaza. Watu mashuhuri pia wanalea watoto waliovunjika, kwa sababu yenu wanyanyasaji, mnatunyanyasa, mnanyanyasa familia zetu, mnanyanyasa watoto wetu, yani ubinadamu uliondoka mitaa hii. Haki ya watu wa mtandaoni inatia uchungu. Wote ni wa kusikitisha, na wanaojipenda, wanaosababisha watu maumivu kushoto katikati ya kulia," mwimbaji huyo alilalamika.

Aliendelea kusema kwamba angechukua hatua ya kisheria dhidi ya watu ikiwa familia yake inashambuliwa kama kile kinachofanywa kwa familia ya Bahati.

“Nimekasirika sana. Kuweni na heshima kidogo kwa familia haswa watoto. Washambulieni Bahati na Diana ndio rika zenu,” alisema.

View Comments