In Summary

•Shakilla Tifanny ameweka wazi kuwa anapendelea kuchumbiana na wanaume wa Nigeria kuliko wanaume wa Kenya.

•Shakilla hakusita kukiri kuwa yeye ni ‘gold-digger’ na alithibitisha kwamba anapenda kuomba pesa kutoka kwa wanaume.

Image: INSTAGRAM// SHAKILLA

Mwanasosholaiti wa Kenya, Shakilla Tifanny ameweka wazi kuwa anapendelea kuchumbiana na wanaume wa Nigeria kuliko wanaume wa Kenya.

Katika mahojiano na Mpasho Alhamisi jioni, mrembo huyo mwenye umri wa miaka 23 alidokeza kuwa ana sababu nyingi kwa nini hapendi wanaume wa Kenya.

Miongoni mwa sababu alizotoa, alidai kuwa wanaume wa Kenya hawatoi pesa zao kirahisi, hawana sura nzuri na hawadumu muda mrefu kitandani.

"Wanaume wa Kenya ni wastingy, wanafanana, hawana sura nzuri," Shakilla alisema.

Aliongeza, "Ninasisitiza sana neno 'stingy'. Wanaume wa Kenya hawawezi kamwe kukupa pesa, afadhali akulipe kuliko kukupa pesa. Alafu hawadumu kitandani, hawadumu, ni dakika! Ninazungumza kuhusu masaa na Nigeria."

Mwanasholaiti huyo mwenye umri wa miaka 23 pia alidai kuwa wanaume wengi Wakenya wako kwa ndoa na inambidi anayechumbiana naye awafiche ilhali yeye anataka kuonekana na mume wake na kumuonyesha.

“Mwanamume Mkenya hawezi kukugharamia ndege. Watalazimika kukuuliza maswali milioni moja kabla ya kukubali hilo," alisema.

Shakilla hakusita kukiri kuwa yeye ni ‘gold-digger’ na alithibitisha kwamba anapenda kuomba pesa kutoka kwa wanaume.

"Nitaomba pesa kila wakati, nimesota. Kwa kweli sina pesa kabisa unaponiona hivi. Ndio, mimi ni gold digger,” alisema.

Mwanasosholaiti huyo alidokeza kuwa ana thamani ya zaidi ya Ksh2milioni.

Alipoulizwa ni wanaume wangapi amewahi kulala nao, alibainisha kuwa hana uhakika sana kwani si rahisi kwake kuwahesabu.

"Nadhani niko chini ya 100, chini ya 150." Alisema.

Aidha, alibainisha kuwa tayari amelala na wanaume wengi mwaka huu

"Sijalala na mtu yeyote tangu Februari," aliongeza.

View Comments