In Summary

•Wahu alilazimika kujibu baada ya wanamitandao kumpongeza kwa madai kuwa ana ujauzito wa mtoto wake wa nne.

•Huku akijibu, Wahu alionekana kukanusha uvumi wa kuwa mjauzito na kudokeza kuwa alikuwa ameshiba tu baada ya kula chakula.

Wahu na mume wake Nameless wakati wa hafla ya King Kaka.
Image: INSTAGRAM// KING KAKA

Mwanamuziki maarufu wa Kenya Wahu Kagwi alilazimika kujibu baada ya wanamitandao kumpongeza kwa madai kuwa ana ujauzito wa mtoto wake wa nne.

Mwimbaji mwenzake, Kennedy Ombima almaarufu King Kaka alikuwa ameshiriki picha yake na mumewe Nameless akiwapongeza kwa kuhudhuria hafla yake ya ‘Opulence in the City’ wakati wanamitandao walipopata shauku ya kutaka kujua hali ya mama huyo wa watoto watatu.

"Mshawishi wangu @nameleskenya na rafiki yangu mzuri @wahukagwi walipamba ukumbi wa Coliseum. Opulence in the City,” King Kaka aliandika kwenye Instagram

Katika sehemu ya maoni ya chapisho hilo, wanamitandao  wengi walihoji iwapo mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43 ni mjamzito kwa mara nyingine chini  ya mwaka mmoja au alikuwa ameshiba tu kutokana na kula chakula. Wengine hata waliendelea zaidi kumpongeza wakisisitiza kwamba anatarajia mtoto wake wa nne.

Huku akiwajibu wanamitandao, Wahu alionekana kukanusha uvumi wa ujauzito na kudokeza kuwa alikuwa ameshiba tu baada ya kula chakula.

"Watu watu, msichana anaweza kufurahia chakula chake kwa amani bila pongezi yawa?," Mke huyo wa Nameless aliandika.

Tazama baadhi ya maoni ya wanamitandao;-

@rachealnyambu: Ababy boy loading congratulations 🎊 👏 💐 the methenges😍

@jay_maimah_ Baby number 4 @kisunzy_swaleh: Najuwa mnaogopa kuuliza kama wahu ako na ball

@paskagiyo: Hii ndio comment you all mnatafuta wahu ni kushiba ameshiba alo stress free na food.

Zablovincent: Wahu ako fiti, tukutane hapa after 7 months niwape majibu

@Chalisterjudy: Sasa hapo kwa baby gal kukula inategemea nini. Anyways inakaa anakula vifitiii. period sindio @wahukagwi.

miss_moniks: Guys, Wahu just had a baby! Loosing baby weight takes time.

leahmusyra: Hana mimba nikuwekwa vizuri.. this the coom

View Comments