In Summary

•Baada ya kiongozi wa kanisa la new life prayer center kutoa madai ya wanadada wenye jina Diana kutofanikiwa kwenye ndoa wakenya mbali mbali wametoa maoni kuhusiana na jambo hili

Viongozi wa makanisa nchini wameshauriwa kuwa makini na matamshi wanayotoa kwa sababu yana athari sana kwa jamii. 

Kiongozi wa kanisa la Life Church Limuru  pasta T Mwangi amekosoa matamshi ya pasta Ezekiel Odero kuhusu jina Diana. 

Pasta Odero katika mahubiri yake alionekana kudhalilisha jina Diana akisema kwamba wasichana wote wenye jina hilo wanakabiliwa na changamoto nyingi katika mahusiano yao.

Kulingana na kauli hii pasta Mwangi alisema kuwa hayo ni maoni ya pasta Ezekiel tu ,huku akitaka viongozi wa makanisa kuchunguza maneno ambayo wanasema katika ibada zao.

"Naomba kila mtu achunguze kile anachosema kwa jamii kwa maana siku hizi Tecknolojia ipo na inafanya kazi kwa minajili ya kufahamisha watu matukio yanapojiri kwa hivo mtu anaweza kusema maneno na wengine wachukulie kuwa jambo muhimu ' alisema pasta T mwangi.

Pasta T Mwangi aliwatetea wanadada wenye majina Diana ambao kulingana na kauli ya pasta Ezekiel yeyote mwenye jina Diana kwa maisha yake hawezi kaa kwa ndoa.

Kiongozi huyu wa kanisa la Life Church Limuru alipeana mfano wa watu mashuhuri ambao walikuwa na jina Diana na walifanikiwa katika ndoa akipeana mfano wa Malkia Diana.

Ezekiel Odero na ambaye ndiye mwazilishi wa kanisa la New Life Prayer Center ambalo liko Mavueni katika kaunti ya Kilifi  alisema maneno haya alipokuwa na ibada na washirika wake

Mhubiri Ezekiel ameshawishiwa na pasta wa kanisa la life church kuyasafiha maneno yake kwa kuwa ni kiongozi na ambaye amekuwa na wafuasi wengi ambao wanachukua mfano wake na kutilia kila jambo asemalo maanani .

Pasta Mwangi kupitia kikao na wanahabari alidokeza kuwa hata Rais anafaa kuchuja semi zake. 

 

View Comments