In Summary

• Rigtone kwenye mahojiano haya aliweza kuzugumuzia mambo kadhaa ikiwemo kuuza gari lake baada ya bei ya mafuta kuwa ghali.

Image: INSTAGRAM// RINGTONE APOKO

Msanii wa nyimbo za injili wa  Kenya Ringtone Apoko katika mahojiano aliyofanyiwa nyumbani kwake amefunguka na kusema kuwa yeye hana pesa na utajiri wake uko mbinguni .

Rigtone kwenye mahojiano haya aliweza kuzugumuzia mambo kadhaa ikiwemo kuuza gari lake baada ya bei ya mafuta kuwa ghali.

'Niliishiwa siku hizi naenda na mguu ,ni vizuri pia kuwa na uzoefu wa kutembea kwa miguu kama vile wakenya wengine hufanya ,niliuza gari langu baada ya bei ya mafuta kuwa ghali niliona sitatumia pesa nyingi kwa mafuta tu na nikaaamua kuuza gari langu,' Rigtone alisema.

 Wakati wa mahojiano haya Msanii huyu alitaja kugadhabika kwake kuona msanii mkubwa wa injili kutoka Tanzania Christina Shusho wakati alipokuwa anazuru Kenya alikaribishwa na Eric Omondi ,Ringtone alimtaja Eric Omondi kuwa msherati na hangefaa kukumbaliwa kumkaribisha msanii wa injili nchini.

'Nashangaa Eric Omondi anampokea Christina Shusho kwa nini wakati ambapo wasanii wa nyimbo za injili wapo Shusho angekumbali kukaribiswa na Eric ambaye anapenda raha ya dunia kuliko mungu cha kusitikisha anavaa nguo kama mwanamke na anatembea uchi naudhika sana' msanii Ringtone alisema.

Ringtone hata hivyo aliwataja wasanii wa nyimbo za injili kukosa maandili na ambao wamejiingiza kwa mambo ya usharati na hivo msanii huyu ametaja wasanii wa injili kuwacha kuvaa nguo za wanawake.

Mwimbaji huyu alifichua kuwa yeye kwa sasa anatumia muda mwingi sana kwa maswala ya kusoma bibilia.

View Comments