In Summary

• Alikuwa ameweka sinia kubwa la wali uliopikwa vizuri kwa viungo ainati na kando ya kile kilionekana kama meza kulikuwa na vinywaji chupa mbili.

Jamaa akila na mbuzi wake
Image: tiktok

Video inayomuonesha mwanamume mmoja akiwa ameketi barazani akila wali na mbuzi wake kutoka sahani moja imezua vichekesho katika mtandao wa TikTok.

Video hiyo ilipakiwa kwenye ukurasa kwa jina Ogaemma Update na ilimuonesha mwanamume huyo mwenye umri wa makamo alifurahia chakula chake nje ya nyumba yake.

Alikuwa ameweka sinia kubwa la wali uliopikwa vizuri kwa viungo ainati na kando ya kile kilionekana kama meza kulikuwa na vinywaji chupa mbili.

Kilichowashangaza wengi, mbele yake alijumuka naye mbuzi wa rangi ya ngozi nyeusi ambaye alikaribia bila kuogopa na kujiunga na jamaa huyo kwa msosi.

Jamaa huyo wala hakuonesha kughadhabishwa au kuwa na athari vyoyote kutokana na kushiriki sahani moja kwa mlo na mbuzi wake.

Kila mmoja – mbuzi na jamaa huyo – walionekana kuchukua zamu yao kwa kubugia wali mdomoni huku akitabasamu kwenye kamera.

Baadhi ya watu walioona video hiyo walimsifia jamaa huyo kwa ukaribu na urafiki wake na wanyama wa kufugwa nyumbani huku wengine wakisema kwamba wanyama wa nyumbani siku zote ndio marafiki nambari moja kwa mwanadamu.

Haya hapa ni maoni ya watu walioshiriki katika klipu hiyo ya TikTok;

Joachim Chenyi: “Baada ya kukatishwa tamaa na marafiki ndugu familia unakua unaelewa wanyama wanaweza kuwa marafiki bora na wa kweli.”

Dorcas Daniel9263: “Hii ndio njia bora ya kuisjhi sasa😌 dunia ni mbovu ukijiweka karibu na binadamu.”

Robert Zack: “Mwacheni mwacheni amlishe Messi kwa ajili yangu tafadhali Messi anahitaji chakula pia.” Alisema akirejelea jina la kumsifia mchezaji namba moja duniani.

Sandra: “Labda amekuwa akila na marafiki-maadui akagundua tu kuwa wanyama ni bora kuliko wanafiki.”

Expensive CommenterGH: “Kuwa na uhusiano wa karibu na kihisia na chakula chako ni kiwango kingine cha furaha😁”

View Comments