In Summary

•Chira alibainisha kuwa aliomba msamaha kwa Nyako na TikToker Baba Talisha kwani wote walimsaidia kupata pesa

Brian Chira na TikTiker Nyako Picha/Instagram

Mtayarishaji  maudhui Brian Chira  hatimaye amemuomba radhi Wanatiktok Nyako  na Baba Talisha baada ya kuwarushia  matusi .

Haya yanajiri baada ya TikToker Nyako kusaidia kuchangisha takriban Sh 500,000 kwa aliyekuwa mtangazaji Kimani Mbugua.

Chira alibainisha kuwa aliomba msamaha kwa Nyako na Baba Talisha kwani wote walimsaidia kupata pesa.

“Naitwa Chira, Brian Chira, na kwa muda wa siku tatu zilizopita, mengi yameendelea katika maisha yangu, ninachoweza kuwaomba ni mnisamehe.Mama Nyako na Baba Talisha, tafadhali nyie ndio mnanielewa zaidi. Fungua moyo  mnisamehe."

 Chira alimkashifu TikToker Nyako mtandaoni wiki kadhaa baada ya kumpa mkono na kumsaidia kutafuta nyumba mpya.

Nyako alikuwa ameona jinsi mtayarishaji wa maudhui alivyokuwa akihangaika licha ya kujipata matatani kwa kuwatusi watu kwenye mitandao ya kijamii. Alimfanyia Chira harambee na kumhakikishia kuwa atamsaidia na hata akaapa kutafuta njia ya kumpeleka Ulaya.

"Tutaanza na sehemu ya kukaa ili uwe imara, nyumba imara ndio kitu cha muhimu kwako kwa sasa. Sehemu unayoita nyumbani hata kama ni chumba kimoja. Lakini unajua nikienda huko, Nitakuwa na amani ya akili kuliko leo uko hapa,"  Nyako alisema

Chira hata hivyo hakuonyesha heshima kwa Nyako kwani alitoa maneno ya kumdhalilisha kwenye ukurasa wake wa TikTok .

Brian alibainisha kuwa Nyako hakuwa mama yake wala hakumjali.

"Si mama yangu hanijali, unafikiri mimi  ninamjali Nyako? Nilie juu ya kodi? Duniani kuna watu bilioni sita. Kwani ni yeye pekee anayeweza kunizawadi? Watu walikuja na kuondoka Siombi rent, Nyako ukiskia kama utalipa rent ya mwezi huu utalipa na kama hutaki uwache unafikiri ninajali, sina deni lako,” alisema.

View Comments