In Summary

•Kajala alishare ujumbe akidokeza kwamba amepata mwanamume ambaye anamtaka na kubainisha kwamba ameridhika. 

•Mastaa hao wa bongo walikuwa wamerudiana mwezi Mei mwaka uliopita baada ya kutengana mwaka mmoja kabla.

Image: INSTAGRAM// FRIDA KAJALA

Muigizaji mkongwe wa Tanzania, Frida Kajala Masanja amedokeza kuhusu mahusiano mpya. 

Mama huyo wa mtoto mmoja wa kike mnamo Jumatano alishare ujumbe akidokeza kwamba amepata mwanamume ambaye anamtaka na kubainisha kwamba ameridhika. 

“Nimepata mwanaume ninayemtaka, nimefurahi,” ujumbe huo ulioshirikishwa na Kajala kwenye Instastori ulisomeka.

Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 40 hata hivyo hakushiriki maelezo zaidi kuhusu mahusiano yake mapya au mwanaume ambaye amechukua nafasi ya Harmonize. 

Haya yanajiri takriban miezi kumi baada ya uhusiano wake na bosi wa Konde Music Worldwide kufika kikomo baada ya kuchumbiana miezi kadhaa. Mastaa hao walikuwa wamerudiana mwezi Mei mwaka uliopita baada ya kutengana mwaka mmoja kabla. Harmonize alifanya juhudi nyingi kumuomba msamaha Kajala na kumtongoza katika juhudi za kumshawishi akubali kufufua uhusiano wao uliovunjika.

Image: INSTAGRAM// KAJALA FRIDA

Wakati akitangaza kuachana na mwanamuziki huyo mwezi Desemba, Kajala aliweka wazi kwamba alikuwa tayari kupiga hatua nyingine baada ya mahusiano yao ya miezi michache kugonga mwamba.

Ingawa hakufichua kilichowatenganisha, aliweka wazi kwamba hakubeba kinyongo chochote dhidi ya mwimbaji huyo.

"Mimi kama mwanamke na binadamu nimeumbwa kupenda na kusamehe pia, ila kwenye hili nastahili kuchekwa, nastahili kubezwa na kudharauliwa pia. Sipo hapa kujitetea wala kutia huruma ni kweli nilifanya makosa na nimeyagundua makosa yangu, mimi siyo mkamilifu," Kajala alisema wakat huo.

Wakati wa mahojiano na kituo cha redio cha hapa nchini mapema mwaka huu, Kajala alidokeza kuwa alimtema Harmonize kwa sababu ya mazoea.

"Sijui niseme nini. Labda mazoea. Mtu akishakuzoea sana anakuchukulia poa," alisema.

Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 40 alidokeza kwamba Harmonize bado hakuwa tayari wakati alipoamua kutulia naye kwenye mahusiano na kuwa huenda alihitaji nafasi ya kufanya mambo yake binafsi.

"Yaani mimi hata simlaumu, kwa sababu yeye ni kijana mdogo. Labda alihitaji nafasi, tulikuwa tuko karibu sana.

Yeye mara ya kwanza nahisi labda aliona kama mzaha akisema nataka huyu mtu, nataka niwe naye 24/7.  Mnaamka wote mnaenda gym, mnafanya hiki na kile. Labda alikuwa anahitaji nafasi yake afanye vitu vyake," alisema.

Kajala alibainisha kwamba alikubali kurudaina na bosi huyo wa Konde Music Worldwide kwa kuwa bado alikuwa anampenda.

View Comments