In Summary

•Video yake ilivutia sana Wakenya ambao walikuwa na shauku ya kutaka kujua kasisi huyo alikuwa nani na alitoka wapi. Hili lilizua tafrani miongoni mwa Wakenya, ambao walipata akaunti ya TikTok ya kasisi huyo na kuanza kueleza hisia zao kwa mtu wa Mungu.

Kasisi Karabo

Kasisi wa Afrika Kusini amekuwa msisimko usiotarajiwa nchini Kenya, kutokana na video za mtandaoni za TikTok zinazo onyesha akicheza na kujiburudisha wakati wa misa.

Karabo Lephuthing, anayejulikana kama @karabopapak kwenye Tiktok, amewavutia watazamaji wa Kenya kwa sura yake nzuri na maudhui yanayohusiana.

Video zake zinamuonyesha akicheza kwa sauti maarufu za TikTok na kufurahiya wakati wa misa, jambo ambalo limewasisimua waumini wake na wanawake wa Kenya vile vile.

Risper Njeri, mtumiaji wa TikTok, alishiriki video ya kasisi huyo akiimba kwa utani wimbo maarufu wa Kikatoliki "Twende sote nyumbani mwake" kwenye madhabao.

Video yake ilivutia sana Wakenya ambao walikuwa na shauku ya kutaka kujua kasisi huyo alikuwa nani na alitoka wapi. Hili lilizua tafrani miongoni mwa Wakenya, ambao walipata akaunti ya TikTok ya kasisi huyo na kuanza kueleza hisia zao kwa mtu wa Mungu.

Wanawake wa Kenya wamekuwa wakimiminika kwa wingi katika akaunti ya Karabo ya TikTok, wakionyesha mapenzi yao makubwa kwa kasisi huyo. Wengine wamefikia hatua ya kueleza nia yao ya kusafiri hadi Afrika Kusini ili kuhudhuria ibada za kanisa lake.

Wengine wamependekeza kwa mzaha kuwa watawasiliana na Rais William Ruto ili kumwalika kasisi huyo aje kuwabariki waumini wa Kenya.

Mtumiaji mmoja wa TikTok alitoa maoni, "Jewel's_Lina: Kanisa hili liko wapi?"

Mtumiaji mwingine, Sonnie, alisema, "Ruto tunahitaji mtumishi  huyu wa Mungu kuwaombea wanawake wetu tafadhali na tunaahidi tutabadilika kabisa."

Abby@123 pia alitoa maoni yake akisema, "Kwa heshima zote mtu wa Mungu unaweza kufanya misa takatifu katika uwanja wa Kasarani, kwani tunakuhitaji ufanye muujiza nchini Kenya."

Dansi na roho ya furaha ya Kasisi pia imewasisimua waumini wake, ambao wameshiriki video nyingi zinazomuonyesha akifanya kile anachopenda.

View Comments