In Summary

• Wengi walifurahishwa na suluhu za kukabiliana na wizi hata hivyo wengi walishtushwa kwamba watu wangekuwa na ujasiri wa kuiba chakula.

• Mwanamke huyo aliwahi kuwakabili wenzake kuhusu kukosa chakula chake hata hivyo hakuna aliyejitokeza huku uhalifu na wizi ukiendelea.

Mfuko wa chakula uliofungwa.
Image: X

Mwanamke mmoja amewashangaza wafanyikazi wenzake ofisini baada ya kufika kazini akiwa na mfuko wa chakula chake ambao ameutia kufuli kubwa kama njia moja ya kuwazuia kuiba chakula chake.

Kwa mujibu wa haditih hiyo iliyoangaziwa na Daily Mail, mwanamke huyo wa Australia alikuwa anadai kwamba wenzake walikuwa wanadokoa chakula chake wakati hayuko.

Wengi walifurahishwa na suluhu za kukabiliana na wizi hata hivyo wengi walishtushwa kwamba watu wangekuwa na ujasiri wa kuiba chakula.

Mama huyo alikuwa anamnunulia mwanawe chakula akienda naye kazini lakini kila mara alikuwa anapata sehemu kubwa ya chakula hicho kikiwa kimedokolewa na alishuku kuwa mmoja wa wafanyakazi wenzake ndiye aliyehusika na kutoweka kwa chakula.

Mwanamke huyo aliwahi kuwakabili wenzake kuhusu kukosa chakula chake hata hivyo hakuna aliyejitokeza huku uhalifu na wizi ukiendelea.

“Hili ndilo suluhisho langu - begi la Woolies la shili ngi 150 na kufuli. Nilipata kufuli nne kwa $6. Kwa hivyo kwa $10 nina mifuko minne inayoweza kufungwa,” alisema.

Tangu atumie mabegi na kufuli, alisema hajaibiwa au kupoteza chakula.

"Nimefurahi sana kwa hivyo nilitaka kushiriki wazo hili ikiwa mtu mwingine yeyote atakuwa na shida yangu na anaweza kutumia suluhisho langu," mama huyo aliongeza.

 

View Comments