In Summary

• Lakini je, ni kweli kwamba mwanamke hawezi shika mimba kwa kushiriki tendo la ndoa kwa dakika moja tu na kutumia mtindo mmoja?

• Kisayansi, kila wanaume wanapomwaga manii hutoa karibu mbegu milioni 100 na mwanamke ana uwezo wa kupata mimba haijalishi ni muda upi wamefanya mapenzi.

Kiwango cha mbegu za uzazi za kiume kilianguka kwa 51% katika kipindi cha miongo mitano, kulingana na tafiti
Image: BBC

Mwanamume mmoja ameiacha mahakama katika vichekesho vikali baada ya kusimulia sababu zake za kuikataa mimba ya mpenzi wake ambayo ni ya watoto watatu.

Kwa mujibu wa klipu ya video ambayo imekuwa ikienezwa mitandaoni, mwanamume huyo mwenye umri wa makamo aliburuzwa mahakamani na aliyekuwa mpenzi wake.

Mrembo huyo alikwenda mahakamani akidai kwamba anatarajia watoto watatu lakini mhusika alikuwa ameikataa mimba hiyo si yake.

Aliitaka mahakama kumshurutisha mhusika huyo kuwajibika moja kwa moja kwa mimba lakini pia kushughulikia watoto watarajiwa.

Maelezo ya mwanamume huyo mahakamani hata hivyo yaliwaacha wengi katika vichekesho, kwani ni maelezo ambayo hayakuwa yanatarajiwa kabisa.

Jamaa huyo alieleza mahakama kwamba ana sababu kuu tatu za kuikataa mimba hiyo; moja ni kwamba walishiriki tendo la ndoa kwa raundi moja pekee, pili walitumia mtindo mmoja tu wa kufanya mapenzi na tatu walifanya mapenzi chini ya sekunde 60 na hivyo haina mantiki yoyote kwamba mrembo angeshika mimba – tena ya mapacha watatu!

Lakini je, ni kweli kwamba mwanamke hawezi shika mimba kwa kushiriki tendo la ndoa kwa dakika moja tu na kutumia mtindo mmoja?

Kisayansi, kila wanaume wanapomwaga manii hutoa karibu mbegu milioni 100, hata hivyo, mapacha watatu wanaofanana hutoka kwenye yai moja ambalo limerutubishwa na mbegu moja kabla ya kugawanyika na kuwa tatu.

Pande tatu zisizofanana huundwa wakati mayai matatu tofauti yanaporutubishwa na mbegu tatu tofauti.

Hii ina maana kwamba wakati mwanamume na mwanamke wanapatana kimwili, kutolewa kwa mbegu na mwanamume kunaweza kusababisha mwanamke kuwa na mimba ya 1 au 2 au 3 au zaidi.

Na mimba inaweza ikaingia pindi tu mwanamume anapoachilia mbegu zake, haijalishi ni ndani ya sekunde, au dakika ngapi.

 

View Comments