In Summary

•Mwanamume huyo alidokeza kuwa walimu wengi wa hesabu huwaonya wanafunzi wao kwamba wale ambao watafeli katika somo hilo hawatafika mbali kitaaluma.

Hisabati
Image: BBC NEWS

Mkenya mmoja ambaye ameonekana kughadhabishwa na kauli ya mzaha ya ‘Mwalimu wa Math hapa ni wapi?’ ameiandikia barua tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa NCIC akitaka kuharamishwa kwa kauli hiyo kwa kile anasema ni kauli ya kuchochea uhasama.

Waraka wake ulionekana kwenye gazeti moja la humu nchini. William Wainaina kutoka Migori aliandika kwa kuelezea sababu kadhaa ambazo zimempelekea kufikiria na kugundua kwamba kauli hiyo si ya kuleta heshima kwa walimu wa somo la hisabati shuleni.

Mwanamume huyo alidokeza kuwa walimu wengi wa hesabu huwaonya wanafunzi wao kwamba wale ambao watafeli katika somo hilo hawatafika mbali kitaaluma.

Kufeli katika hesabu, kwa hivyo, ni sawa na kufeli maishani. Maneno haya yaliwaudhi sana wanafunzi hadi ikatungwa kauli "Mwalimu wa Math", Wainaina alisema katika sehemu ya waraka huo.

Ucheshi wa kutopenda na kejeli za walimu wa hisabati ulikuwa uumbaji wa awali wa askari wa Kenya. Katika video ya kuchekesha iliyosambaa mitandaoni, askari huyo na wenzake wawili waliwakejeli walimu wao wa hesabu, wakisema walikuwa wametabiri kwamba wangefeli, labda kwa sababu ya uwezo wao duni wa masomo.

Watatu hao, wakiwa wamevalia gia za kijeshi na wakiwa wamebeba bunduki, walirekodi video ya TikTok katika eneo lililoonekana kutostaarabika ambapo walidaiwa kwenda kufanya operesheni ya kijeshi.

Huu hapa ni waraka huo kama ulivyopigwa picha kwenye gazeti hilo;

View Comments