In Summary

•Bi Maria Cataleya kwenye Tiktok alieleza kuwa alitumai Rosie atarudi lakini moyoni mwake anatumai hatarudi.

•Maria alieleza kwamba anahisi video yake ya mtandaoni inaweza kufungua milango kwa fursa bora kwa Rosie nje ya Lebanon.

Rozzie akiondoka Lebanon
Image: HISANI

Bosi wa Roseline ‘Rosie’ Atieno ametoa video inayoeleza kwa nini hataki msaidizi huyo wake wa nyumbani arudi Lebanon kwa sasa.

Bosi wa Atieno, aliyetambuliwa kama Maria Cataleya kwenye Tiktok alieleza kuwa alitumai Rosie atarudi lakini moyoni mwake anatumai hatarudi. Kwanini unauliza? Kweli Maria ni mtu wa kibinadamu kabisa ....

"Bila shaka, natumai atarudi. Lakini sidhani hivyo. Ni kama sitaki arudi. Nataka afurahie wakati wake na watoto wake na labda abaki nao," Mwanamke huyo wa Lebanon alisema katika video ya TikTok ambayo imekusanya zaidi ya watazamaji milioni 2.4 na kupendwa zaidi ya 106.1k saa 24 baada ya kuchapishwa.

Mama huyo wa watoto 4 aliendelea kuongeza; "Kama ningekuwa yeye, ningebaki Kenya na watoto wangu. Nisingerudi Lebanon, lakini ni juu yake."

Maria aliendelea kueleza waziwazi kwamba anahisi video yake ya mtandaoni inaweza kufungua milango kwa fursa bora kwa Rosie nje ya Lebanon.

"Nina uhakika baada ya video hii ya mtandaoni, ataweza kupata fursa nyingine bora kuliko kurudi Lebanon," mwajiri wa Rosie alitoa maoni.

Rosie na mwajiri wake walipata umaarufu siku chache zilizopita baada ya kusambazwa kwa video yake ya hisia akiaga familia ya mwajiri wake kutoka Lebanon. Alikuwa akifanya kazi Lebanon kwa miaka miwili iliyopita,

View Comments