In Summary

•Harmonize alidokeza uhusiano wake hauhusishi kufichana mambo yoyote akisema mwanamke anayechumbiana naye huwa na simu yake wakati mwingine.

•Bosi huyo wa Konde Music Worldwide alijigamba kuhusu kuwa mpenzi mwaminifu kwa mpenzi wake.

Harmonize akibarizi na Poshy Queen
Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul Kahali almaarufu kama Harmonize ameendelea kumsifia mpenzi wake wa sasa na kutoa maelezo kuhusu uhusiano wao unaoonekana kuwa mzuri.

Katika chapisho lake la Instagram siku ya Jumatatu, bosi huyo wa Konde Music Worldwide alijigamba kuhusu kuwa mpenzi mwaminifu kwa mpenzi wake.

Aidha, alidokeza kuwa uhusiano wake mpya hauhusishi kuficha mambo yoyote akifichua kuwa mwanamke anayechumbiana naye huwa na simu yake wakati mwingine.

"Mwanaume mwaminifu ulimwenguni! Mpenzi wangu huenda na simu yangu ya rununu, tayari ana password ya simu yangu. Iwapo utapata jibu lisilo la kawaida, bado nina upendo nanyi nyote,” alisema Harmonize kupitia Instastories yake.

Mwanamuziki huyo alifichua kuwa alitaka kuchumbuina na mpenzi wake kitambo lakini uhusiano wao haukufaulu wakati huo kama walivyokusudia.

Aidha, aliendelea kutangaza kuwa sasa ametulia kwani mwanamke anayetoka naye sasa hivi atakuwa wa kudumu kwake.

“Hapa ndio mwisho wangu. Onyoo, hajawahi kutembea na yeyote ninayemjua. Mheshimu kama msichana wangu. Popote utakapomuona uache drama!” alisema.

Taarifa hii inakuja siku chache baada ya msanii huyo wa zamani wa WCB kudokeza kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanasosholaiti maarufu wa Tanzania, Poshy Queen.

Wiki iliyopita, mastaa hao wawili walionekana wakiwa pamoja kwenye boti na walionekana kushiriki nyakati nzuri za kimapenzi.

"Leo na mtu iliyeongelewa zaidi sana Tanzania mwaka wa 2024 @poshyqueen. Sahau kuhusu sauti hiyo kubwa tunayosikilizia, naweza kumuweka kwenye mojawapo ya video yangu? Au nimuoe tu kama wanavyodhania,” aliandika Harmonize chini ya video hiyo aliyoishiriki Instagram.

Siku ya Jumatatu, mrembo huyo pia alichapisha picha ya bosi huyo wa Kondegang na kumtambulisha kama "Adam wangu mimi hapa."

View Comments