In Summary

•Phil aliweka wazi kuwa yeye na mzazi mwenzake walikubaliana kuhusu kuuza gari hilo kabla hata hajachukua hatua hiyo.

•Kate Actress kwa upande wake aliwataka waenezaji wa habari za uongo kufanya jambo la maana na nguvu zao.

Kate Actress na Director Phil
Image: Insta

Muigizaji mashuhuri wa Kenya Catherine Kamau almaarufu Kate Actress anaonekana kukubaliana na kauli ya aliyekuwa mume wake Philip Karanja kuhusu suala la gari ambalo mkurugenzi huyo wa filamu alimpa kama zawadi baada ya kujifungua.

Siku ya Jumatatu asubuhi, Philip Karanja ambaye ni maarufu kwa jina la Phil Director alitoa taarifa akikanusha madai ya kuuza gari hilo kufuatia uvumi ambao umekuwa kwenye mitandao ya kijamii hivi majuzi.

Mapema mwezi huu, madai yaliibuka kuwa muigizaji huyo wa zamani wa Tahidi High alichukua kwa nguvu umiliki wa gari hilo la kifahari ambalo alimzawadia Kate kufuatia kuzaliwa kwa binti yao na kuliuza.

Hata hivyo, huku akikanusha madai hayo, mwanzilishi huyo wa kampuni ya Phil-It Productions aliweka wazi kuwa yeye na mzazi mwenzake walikubaliana kuhusu kuuza gari hilo kabla hata hajachukua hatua hiyo

"Najua Udaku Hukuwa Tamu lakini hata hivyo wacheni hadithi za uwongo," Phil alisema katika taarifa aliyoitoa kupitia akaunti yake ya Instagram.

Aliongeza, “Ninaelewa kwamba blogu zinapaswa kuuzwa na mmejifurahisha. Ningependa kuandika rasmi kwamba gari liliuzwa kwa ridhaa ya pande zote mbili na hakuna mabishano na Kate kinyume na taswira yoyote inayopendekeza vinginevyo."

Huku akikubaliana na ufafanuzi huo, Kate kwa upande wake aliwataka waenezaji wa habari za uongo kufanya jambo la maana na nguvu zao.

"Tafadhali elekezeni nguvu hizo kwenye kutazama msimu mpya wa Becoming CEO. Hatuhusu maisha hayo poleni na asante," alisema.

Madai kwamba Phil alimnyang'anya Kate gari aina ya BMW alilokuwa amemzawadia yalisambaa baada ya blogu ya eneo hilo kuandika hadithi kutoka kwa mahojiano.

Kulingana na blogu hiyo, BMW X3 ilichukuliwa tena huku Phil akidaiwa kusema alikuwa na majuto kununua gari ambalo lilionekana kuwa ghali sana kulitunza.

"Ninapenda sana magari, na kwa hivyo nilikuwa mdogo na mjinga, na nilitumia pesa nyingi kununua gari langu, na imekuwa safari ya gharama kubwa sana kuitunza. Mimi ni kama, hilo ni gari ambalo ningelitumia kwa busara mahali fulani. Niliiuza. Nimeamua kurejea Uber.

Gari hilo ambalo lina thamani ya Ksh3.5mil lilikuwa zawadi kwa mwigizaji huyo kwa kuzaa binti yao Njeri.

View Comments