In Summary

•Mwanamuziki Akothee ametoa onyo kali kwa washirika wake wa kiume ambao hawaheshimu wakati wake wa faragha.

•Mwimbaji huyo alionya kuwa kwa kawaida huwa yuko bize na meneja huyo wake katika wakati wake wa faragha.

Akothee na meneja wake Nelly Oaks.
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwimbaji na mjasiriamali mashuhuri wa Kenya Esther Akoth almaarufu Akothee ametoa onyo kali kwa washirika wake wa kiume ambao hawaheshimu wakati wake wa faragha.

Katika taarifa yake ya Jumanne, mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43 alibainisha kuwa kuna baadhi ya washirika wake wa kiume ambao wana mazoea ya kumpigia simu na kumtumia meseji wakati tu ambapo mpenzi wake Nelly Oaks yuko karibu.

Kutokana na hilo, mama huyo wa watoto watano alishangaa nia ya wanaume hao huwa ni gani na akawataka waache tabia hiyo.

"Kuna baadhi ya washirika wangu wa kiume ambao hunipigia tu simu na kunitumia ujumbe wakati @nellyoaks yuko karibu. Nia yako ni nini?,” Akothee aliandika kwenye Instagram.

Mwimbaji huyo alionya kuwa kwa kawaida huwa yuko bize na meneja huyo wake katika wakati wake wa faragha na akawataka wanaume wenye tabia ya kumpigia simu kufuta nambari yake.

“Pepo chafu. Niache na ufute namba yangu niko busy na @nellyoaks usinipigie wala kunitumia meseji tafadhali sina muda wa show za pembeni 💪,” alisema.

Bw Nelly Oaks, ambaye jina lake halisi ni Nelson Oyugi ni meneja rasmi wa Akothee na pia anaaminika kuwa mpenzi wake.

Mara nyingi, wawili hao mara wameonekana wakishiriki nyakati nzuri za kimapenzi pamoja hadharani na mara nyingi katika siku za nyuma, Akothee amedokeza kuhusu uhusiano wao.

Takriban miezi iliyopita, mwanamuziki huyo alionekana kuthibitisha kufufuka kwa mahusiano yake na meneja wake wa muda mrefu Nelly Oaks katika kipindi cha moja kwa moja cha hivi majuzi kwenye mtandao wa TikTok.

Katika kipindi hicho ambacho alikuwa akiwahutubia mashabiki wake Nelly Oaks akimwandalia chakula maalum jikoni, Akothee alisikika akimwita meneja huyo wake ‘babe’ mara kadhaa, jina ambalo hutumika sana sana  wapenzi.

Nelly Oaks pia alisikika akimtaja Akothee kama mtu maalum kwake huku wawili hao wakishiriki matukio ya kimapenzi kwenye kamera.

“Hiki ni chakula cha jioni maalum kwa mtu maalum kama wewe. Ni surprise,” Nelly Oaks alisikika akimwambia mwanamuziki huyo.

Wakati wa kipindi hicho, Akothee kwa hasira aliwasuta wanawake wote waliokiri mapenzi yao kwa meneja huyo wake akidokeza kuwa hapatikani kwao.

Wakati baadhi ya mashabiki walipotaka kujua iwapo Nelly Oaks ana mchumba, mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43 alionekana kuthibitisha kuwa yeye ndiye anashikilia nafasi hiyo.

“Ati kama Nelly ako na mtu?! Kwani mimi mawe? Mimi mawe? Ama mimi ni mti? Unauliza kama Nelly ako na mtu, kwani mimi ni mawe? Ama kijiti? Usinipimie pumzi. Maisha ni ya kwangu nayaendesha vile nataka,” alisema.

Mama huyo wa watoto watano pia alikataa ombi la nambari ya simu ya Nelly Oaks huku akifichua kwamba hata ana uwezo wa kufungua na kutumia simu yake.

“Kweli nikupatie namba ya Nelly? unadhani mimi nimetosheka? Mimi sijarudi soko, mimi ndiye soko, sigawani na mtu,” Akothee alisema.

Nelly Oaks pia aliweka wazi kuwa hapatikani kwa mwanamke mwingine.

View Comments