In Summary
  • Wakati alkuwa akiwashirikisha mashabiki wake katika kipindi cha Maswali na Majibu kwenye mtandao wa Instagram, mama wa watoto wawili Asia brown na Ice brown alieleza kuwa aliachia wazazi wake watoto.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Vera Sidika katika mtandao wake wa kijamii ameeleza watu kuwa uhusiano ako nayo na watoto wake ni mkali sana.

Alieleza kuwa muda wake mwingi anautumia na watoto wake maana hana ajira.

Wakati alkuwa akiwashirikisha mashabiki wake katika kipindi cha Maswali na Majibu kwenye mtandao wa Instagram, mama wa watoto wawili Asia brown na Ice brown alieleza kuwa aliachia wazazi wake watoto.

"Uliwaacha wapi Asia na Ice Brown?"  Shabiki mmoja alimuuliza.

Huku akijibu kuwa " Wako pamoja na babu na yaya zao huko Mombasa. Wanafurahia sana huko".

Shabiki mwingine alipongeza jinsi mtoto  wake Ice anavyopendeza.

Kwa upande mwingine, shabiki mmoja alimuuliza jinsi anavyoshughulika na wasiwasi wa kutengana mbali na watoto wake

" Jinsi gani unaweza kukabiliana na kujitenga, wasiwasi mbali na watoto wake?'

Alijibu huku akionyesha screenshot akiwa katika mawasiliano ya video na mtoto wake Ice, " Huyu ni mimi 24/7. Mimi hucheza na wao, kula nao kifungua kinywa,chakula cha mchana na chakula cha jioni kutumia  video. Asia hunionyesha kile amekuwa akifanya na babu yake".

Aliendeleza na kueleza kuwa hajakuwa akilala vizuri kwa sababu ya tofauti ya wakati.

Kuna aliye mpongeza kwa kuzaa watoto wawili na na kurudi kwenye maisha yake ya zamani

Alisema pia ako katika uhusiano wa mapenzina mpenzi wake anayeishi Nigeria lakini  licha hiyo , kwa sasa hayuko kwenye uhusiano wa dhati kwani hakuna majukumu.

View Comments