In Summary

•Bahati alikanusha kuonekana akinywa pombe, akidai kuwa vinywaji vinavyoonekana karibu naye huenda ni marafiki zake.

•Bahati alionekana kushangaa jinsi mama huyo wa watoto wake watatu alivyomharibu kama inavyodaiwa.

Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Mwimbaji wa zamani wa nyimbo za Injili, Kelvin Kioko almaarufu Bahati amejibu madai kuwa mke wake Diana Marua alimharibu kitabia na mienendo.

Bosi huyo wa EMB alizungumza hayo kwenye chaneli ya YouTube ya Diana Marua alipokuwa akijibu swali kuhusu kilichompata baada ya shabiki mmoja kuibua wasiwasi akidai kuwa siku hizi anaonekana kwenye sherehe na eti alianza kunywa pombe, tofauti na siku za nyuma.

“Hey Bahati, siku hizi tunakuona kwa sherehe unachafua meza sana. Kitambo ulikuwa sio mlevi, imekuwaje kwa  Bahati wa kitambo?” shabiki aliuliza.

Mwimbaji huyo wa nyimbo za mapenzi kwanza alikanusha kuonekana akinywa pombe, akidai kuwa vinywaji vinavyoonekana karibu naye huenda ni marafiki zake.

“Mimi, mimi, nachafua meza mimi? Na nini? Na soda, na maji, vitu kama hizo ama chakula? Msichukue vitu vya wengine mniletee,” Bahati alisema.

Diana Marua hata hivyo alimweleza kuwa huenda shabiki huyo alitaka kujua kama kuja kwake katika maisha kulimbadilisha kitabia.

Mwanavlogu huyo alibainisha kuwa kila mara kuna madai kwamba alimharibu walipojitosa kwenye ndoa miaka kadhaa iliyopita.

“Mimi, Diana akaniharibu? Diana alikuwa ameharibika awali. Diana akitaka kwenda out mimi humpeleka,” alisema.

Mwimbaji huyo wa zamani wa nyimbo za injili alionekana kushangaa jinsi mama huyo wa watoto wake watatu alivyomharibu kama inavyodaiwa.

Kwa upande wake, Diana Marua alilazimika kujibu shinikizo la kuokoka kutoka kwa shabiki ambaye alimuonya dhidi ya kutumia dawa za kulevya.

Huku akimjibu shabiki huyo, mtayarishaji huyo wa maudhui wa YouTube aliweka wazi kwamba ana uhusiano wa kibinafsi na mzuri na Mungu.

“Nimeokoka sana. Tusikuje kusema ati juu nimekunywa soda ama nimekunywa nini, eti sina uhusiano na Mungu. Kwamba sitembei na Mungu. Mimi nampenda Mungu sana,” Diana Marua alisema.

Aliongeza, "Hakuna uhuru bora kuliko kuishi maisha bila hofu ya kuhukumiwa. Ninaishi maisha yangu kwa ukamilifu. Mimi wakati tutaenda mbinguni, nitaongelesha Mungu, mimi na yeye. Binafsi.”

View Comments