In Summary

•Meneja wa Stivo alieleza kuwa aliamua kuachana na msanii huyo baada ya familia yake kudaiwa kuanza kuingilia jinsi alivyokuwa akimsimamia staa huyo.

•Meneja huyo aliendelea kufichua kuwa hakuwa amewasiliana na Stivo baada ya familia yake kumchukua.

Image: HISANI

Mwimbaji maarufu kutoka Kibara, Stivo Simple Boy amedaiwa kufukuzwa nyumbani kwake kutokana na malimbikizo ya kodi.

Katika mahojiano ya hivi majuzi, meneja wa Stivo alieleza kuwa aliamua kuachana na msanii huyo baada ya familia yake kudaiwa kuanza kuingilia jinsi alivyokuwa akimsimamia staa huyo.

Anasema mambo yalizuka baada ya Stivo kudaiwa kuzirai wakati wa Mahojiano kwenye runinga ya Citizen wiki chache zilizopita.

Alieleza kuwa baada ya tukio hilo, inadaiwa rapper huyo alichukuliwa na watu wa familia yake ambao walidai kuwa wanamrudisha Kibera.

Aliongeza kuwa alishutumiwa kwa kujinufaisha na Stivo Simple Boy na pesa zake na ndio maana akachagua kujiuzulu kutoka kwa jukumu lake kama meneja.

“Kwanza kabisa, Stivo hakufukuzwa kwa sababu usimamizi wake ulikuwa ukimnufaisha. Alifukuzwa kwa sababu usimamizi ulikuwa unapigwa vita na Stivo pia aliunga mkono wale wanaopigana na meneja wake. Kwa hivyo kama meneja niliacha kukodishwa ili afanye mwenyewe,” meneja alimweleza Mwende Macharia.

Meneja huyo pia alikanusha madai kwamba Stevo alizirai kutokana na njaa alipoonekana mara ya mwisho kwenye Citizen TV kwa mahojiano.

“…Ndugu yake alikuja baada ya tukio la Citizen TV na kusema kwamba alikuwa akimrudisha Kibera. Basi akaenda pamoja naye. Malalamiko yao makubwa yalikuwa kwamba nilikuwa ‘ninakula’ pesa za Stivo, jambo ambalo si kweli,” Chini Boy alieleza.

Aliendelea kusema kwamba lazima alipwe ili kurejesha kurasa za mitandao ya kijamii za Sivo (YouTube, Twitter, na Facebook). Alidai kwamba alinunua kurasa hizo kutoka kwa usimamizi wa zamani wa Stivo na itakuwa ngumu kwake kuzirejesha kwa rapper huyo bure.

Meneja huyo aliendelea kufichua kuwa hakuwa amewasiliana na Stivo baada ya familia yake kumchukua.

Aliongeza kuwa alikataa kulipa kodi ya Aprili kwa nyumba ambayo msanii huyo alikuwa akiishi baada ya kuzorota kwao.

"Nina akaunti za mitandao ya kijamii, nilizichukua kutoka kwa uongozi wake wa zamani na nikawaambia wanapaswa kuzinunua tena. Hawataki Sivo ajizungumzie mwenyewe kwa hivyo nimeamua kubaki nao hadi wawalipe,” meneja huyo aliongeza.

View Comments