In Summary

• Alidai kuwa gharama ya usafiri tayari ni kubwa mno kwa waumini husika kumudu kwa urahisi na bado wanaweza kuchangia kifedha kanisani.

Mchungaji mmoja amekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya video kuenezwa kutoka kwa mahubiri yake akitangaza kusitishwa kwa shughuli za utoaji sadaka katika kanisa lake.

Kwa mujibu wa mchungaji huyo ambaye hajabainika kwa jina, katikati mwa mahubiri yake, alitangaza kwamba shughuli za utoaji sadaka zilikuwa zimesimamishwa katika kanisa lake kwa kipindi cha sasa, akisema kwamba anaelewa fika jinsi waumini wengi wanapitia wakati mgumu kiuchumi kupata pesa.

 Mchungaji huyo aliwarai wachungaji wenzake kutoka makanisa mbalimbali pia kufuata mkondo huo na kuwaondolea waumini mzigo wa kutoa sadaka kwani hali ya uchumi wa nchi ni ngumu na wengi wanapitia nyakati ngumu kupata hata pesa za kununua vyakula nyumbani mwao.

Alidai kuwa gharama ya usafiri tayari ni kubwa mno kwa waumini husika kumudu kwa urahisi na bado wanaweza kuchangia kifedha kanisani.

Kwa maneno yake;

"Hatupaswi kukusanya matoleo leo. Kwa sasa, kwa sababu ya hali ya nchi hii, tunasubiri kutoa. Wachungaji wote wanapaswa kutambua, wakisubiri hali ya nchi hii kuimarika, hawapaswi kukusanya sadaka.”

"Fikiria mtu akija kanisani, akipanda teksi na 1,500 na bado anaacha sadaka, anaweza kuishia kurejea nyumbani. Je, hiyo ni akili? Ikiwa hutaacha pesa, haimaanishi kuwa mchungaji hatakula. Njoo ukamtumikie Mungu wako na uende; mpaka petroli ishuke; Si rahisi.”

Alimalizia kwa kuyataka makanisa mengine kufuata vivyo hivyo, “Kwa wachungaji wote, acheni kukusanya sadaka kwa sasa.”

Tazama video hapa chini…

View Comments