In Summary

•Pritty Vishy anadai msamaha wa video kutoka kwa askofu Kiengei.

•Mashabiki wanasema watamtembelea Kiengei ikiwa atakosa kuomba msamaha kwa njia ya video

Pritty Vishy
Image: Pritty Vishy//Facebook

Mtayarishaji maudhui Pritty Vishy amekataa kukubali msamaha wa askofu Kiengei.

Jumanne asubuhi Kiengei alinyenyekea na kuomba msamaha baada ya video yake kusambaa mtandaoni ambapo alisikika akimtania Simple boy na kumdhalilisha Vishy.

Vishy alionekana kuandika katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram kuwa hatokubali msamaha wake Kiengei ambao alikuwa ameandika. Alisisitiza kuwa anataka msamaha kwa njia ya video jinsi alivyoketi chini na kutengeneza video isiyo na heshima.

"@bishopbenjcchurch ulipofungua mdomo wako na kunitusi ulimtuma msaidizi wako ama ni yeye alikuandikia mistari? kama unataka kuongea na mimi niongeleshe moja kwa moja,na kabla ya hiyo sitaki msamaha wa maandishi nataka video,vivyo hivyo ulikaa chini na kutengeneza video isiyo na heshima, fanya vivyo hivyo kwenye kuomba msamaha...usitume watu kwangu kwani walikusaidia kucheka? ama walikusaidia kupanua mdomo? jiheshimu.

Vishy pia alisema kuwa bado hajamaliza  kulalamika hata kama askofu huyo alikuwa ameifuta video hiyo yeye bado alikuwa nayo.

"kwa watu waliokuwa wakituma meseji kusema askofu wao anatania tu mbona ameifuta video? Nilidhani wote tunatania ama?...Ninayo video na kila mtu anayo...bado sijamaliza"

Pritty Vishi alimalizia na kusema kuwa hajakubali msamaha. Alimuuliza askofu kama aliomba msamaha kwa sababu aliongea na ni kwa nini aliufuta video hiyo kama hakukosea.

'BISHOP "WETU" @bishopbenjcchurch msamaha wako haujakubalika...kama hukukosea kwa nini ufute video? uliomba msamaha kwa sababu nilizungumza sio? msamaha wako haujakubalika hivyo basi wacha aluta iendelee"

Wanamitandao wengi wanamuunga Vishy mkono na kusistiza kuwa askofu huyo anafaa kuomba msamaha kwa video la sivyo watamtembelea askofu kwa kanisa lake siku ya Jumapili.

View Comments