In Summary

•Bradley Marongo ametia saini kama balozi wa unga wa Taifa na Mombasa Maize Millers

•Ameweza kupata nafasi ya kuwa balozi wa makampuni mbalimbali kama vile Khushi Motors,Robimax Auto Trading,Bonfire Adventures,Mombasa Maize Millers na wengine wengi.

Bradley Mtall
Image: Bradley Mtall//Facebook

Bradley Marongo almaarufu Bradley Mtall ametia saini kandarasi kuwa balozi wa unga wa Taifa na Mombasa Maize Millers.

Baada ya kutia saini, Bradley alielezea furaha yake kwa kupata ushirikiano na Mombasa Maize Millers ambao ni wasagaji mahindi nchini Kenya.

'Ninafuraha kutangaza ushirikiano wangu na Mombasa Maize Millers, wasagaji mahindi wanaoongoza katika sekta hii. I look forward to a fruitfull and healthy collaboration. Pamoja, tutahakikisha ya kuwa "Unga Ni Taifa Utakacho Ushapata." @mombasamaizemillers'

Tangu umaarufu, Bradley ameweza kupata nafasi ya kuwa balozi wa makampuni mbalimbali kama vile Khushi Motors,Robimax Auto Trading,Bonfire Adventures,Mombasa Maize Millers na wengine wengi.

Bradley anavyoendelea kupata umaarufu, ndivyo makampuni zaidi yanaendelea kuonyesha nia ya kufanya kazi naye.

Mombasa Maize Millers ni kiwanda kikubwa cha kusaga unga wa mahindi pamoja na ngano nchini Kenya. Chapa zao ni kama vile Taifa,Ndovu,Halisi Fry,Faida Feeds Patco na kadhalika.

Marongo alipata umaarufu baada ya kuonekana wakati wa maandamano jijini Nairobi, urefu wake usio wa kawaida uliwavutia watu pamoja na vyombo vya habari. Tangu wakati huo amekuwa akipata umakini kila mahali anapokwenda.

View Comments