In Summary

•Huddah alitoa masharti magumu kwa mwanasiasa huyo kijana ambaye amekuwa akimmezea mate hadharani kwa muda mrefu.

• Sosholaiti huyo mrembo alichapisha tena jibu la Salasya na chini yake akatoa maoni yake kuhusu ujumbe wa mbunge huyo.

HUDDAH NA SALASYA
Image: HISANI

Mwanasosholaiti mashuhuri wa Kenya Huddah Monroe amejibu maneno matamu ambayo Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya alikuwa ameandika baada ya yeye kutoa masharti ya kuchumbiana naye mwezi uliopita.

Kuelekea mwishoni mwa mwezi Agosti, Huddah alitoa masharti magumu kwa mwanasiasa huyo kijana ambaye amekuwa akimmezea mate hadharani kwa muda mrefu.

Sosholaiti huyo alibainisha kuwa hakutaka wacheza densi kupangwa ili kumchezea kwenye uwanja wa ndege na badala yake akataja alichohitaji.

"Sitaki stori za Isukuti Kwa airport, Shash Lazima na Ksh3.8 milioni za salamu," Huddah alisema alipokuwa akijiandaa kurejea nchini Kenya mwezi uliopita.

Katika majibu yake, Salasya alibainisha kuwa alipokea matakwa ya sosholaiti huyo vizuri na akaweka wazi kuwa yuko tayari kuyatimiza.

Salasya alisisitiza kuhusu upendo wake kwa mfanyibiashara huyo wa vipodozi na akaendelea zaidi kumsifu kwa maneno matamu ya mapenzi.

“Malkia amezungumza, nimemsikia na matakwa yako ni amri yangu @huddahthebosschick wewe bado ningekuchagua. Mpenzi wangu na jumba langu la kumbukumbu, mdundo wa sauti zangu😍," Salsaya alijibu.

“Kwa kila kitu ambacho mpenzi wangu ameomba kwa siku hiyo, tafadhali wasambazaji nitumie DM kwa sababu nataka kufanya oda kubwa kuanzia kwa maua ya machungwa, chupa nyororo za dom na kila kitu kinachohitajika ili sijasema mnikumbushe pia🙈🤣😆😅 na ninafurahi kuona tuna ladha sawa linapokuja suala la starehe unapenda kitu kimoja chenye natumia sana🤣🤣😘,” aliongeza.

Mbunge huyo wa Mumias alidai kwamba yeye na Huddah watakuwa na maelewano mazuri kwani wana mapenzi kwa mambo yanayofanana.

"Siwezi kusubiri kukukumbatia😍nahesabu siku tu!," alisema.

Siku ya Alhamisi, sosholaiti huyo mrembo alichapisha tena jibu la Salasya na chini yake akatoa maoni yake kuhusu ujumbe wa mbunge huyo.

“Mistari bila pesa ni shairi!” Alisema.

Haya yanajiri huku mwanasoshalaiti huyo akiendelea kutoa vidokezo kuhusu kuwa tayari kuchumbiana na mwanasiasa huyo kijana.

View Comments