In Summary

•Bradley ajibu malalamishi ya kuwa amesahau mamake na familia yake

•Alijibu baada ya video kuchapishwa Youtube mamake akisema kuwa hashiki simu zake

Bradley Mtall
Image: Bradley Mtall//Facebook

Bradley Mtall amejibu madai ya kuwa amemsahau mamake mzazi, mkewe na mwanawe.

Bradley anasema kuwa anamtumia mamake pesa na walioenda kumhoji  walimchanganya mamake na maswali na akajibu visivyo. 

"Nilikuwa namtumia pesa, lakini sasa hiyo Murende alienda kumhoji kiujinga sijui alikuwa anataka  tu awaache na viewers ama...so mama akachanganyikiwa ikabidi aongee kitu chochote.. hata akitoka Nairobi nilimpea pesa..." Bradley alisema

Kuhusu kutoshughulikia mwanawe na mkewe, alisema kuwa msichana huyo alipoona hana pesa alitoroka na kuolewa kwingine. Sahii anasema kuwa hamsaidii mtoto.

"Ako, lakini sasa shida ya huyo msichana vile sikuwa na doh, akaamua kutoroka na vile tuliachana na yeye alienda kuoleka kwingine...sahii vile nimeanza kushika elfu tatu, nne, tano hivi, amesema sisaidii mtoto..na ashaolewa"aliongeza.

Trevor alipoulizwa kuhusu malamishi ya kuwa ni yeye anazuia Bradley kuongea na mamake mzazi alijibu kuwa si yeye alikuwa meneja wake Bradley wakati huo ilikuwa marafiki wake wa karibu.

"Kipindi hicho huyo jamaa alisema management inamzuia kuongea na familia,sikuwa around sikuwa nimetake control ya brand ya Bradley...so by that time alikuwa anafanya kazi na vijana wake wale wamegrow naye...hiyo haikuwa mimi ilikuwa marafiki wake tu  wale wa karibu," Trevor alisema.

Trevor anawaomba familia  yake Bradley impe muda kidogo ajitosheleze kwanza ndipo aweze kuwasaidia.

Kwenye video iliyowekwa Youtube, mamake Bradley alisema kuwa Bradley hasaidii familia na kusema kuwa meneja wake hakubali amuongeleshe

"Bradley hata sahii nikipiga simu hashikii..wale manager ako wao wawili wamemshika..si rahisi anipigie simu..nilikuwa Nairobi, wakati mtoto alitoka Mombasa mara ya kwanza, hakuna siku alikanyaga mahali naishi.." mamake alisema.

View Comments