In Summary

• “Ukiwa katika hilo, ningependa kuwaulizeni swali jepesi, kama yeye [mwanamke] angekuwa tajiri na we na vigezo sawia, unafikiri utakuwa chaguo lake?” Yuri aliuliza.

Bravin Yuri
Image: Bravin Yuri//Facebook

Bravin Yuri jamaa anayejitambulisha kama mchanganuzi wa kisiasa kupitia mitandao ya kijamii amedai kwamba utajiri wa wanawake upo katika uwezo wao wa kuonyesha heshima kwa wanaume wao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Yuri alidai kwamba utajiri wa mali ni suala la wanaume kwa sababu wao ndio wanaotafutia na kulisha familia zao.

Kwa upande mwingine, Yuri alisema kwamba mwanamke si sharti awe na mali ya kumilikiwa au pesa ili kuthaminika kwenye ndoa, akisisitiza kwamba ishara ya heshima kwa mwanaume ni utajiri tosha.

"Ni rahisi, kama wewe ndio mwanamume basi ni jukumu lako kutafutia familia. Kama mimi [kama mwanaume] ni tajiri basi moja kwa moja na mwanamke wangu ni tajiri pia. Thamani ya kweli ya mwanamke ni kiwango cha heshima anayo kwa mwanamume wake. Kama mwanamke anakuheshimu kama mume wake basi jua una utajiri wote ambao ungeweza kuhitaji,” Yuri alisema.

Pia aliwasuta wanaume vimbauwau wanaojipiga vifua kwamba hawawezi kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanawake fukara.

Kwa kauli yake, Yuri alisema kwamba mwanamume anayekataa kumpenda mwanamke kisa ni fukara huyo hayuko tayari kuwajibika kama kichwa cha familia bali ni yule mwenye fikira za kugawa majukumu.

“Wakati ukamkuta mwanamue akisema ‘siwezi chumbiana na mwanamke fukara’ kimbia kutoka kwa mtu wa aina hiyo. Huyo ni mtembezi tu anayetaka majukumu kuwa 50/50 na nimewaonya mara si haba,” alisisitiza.

Alimalizia kwa kurushwa swali la balagha kwa wanaume wa aina hiyo akiwataka kujiweka katika nafasi ya wanawake hao na kugeuza kibao wao ndio wawe hawana kitu, je, mwanamke huyo atamuona kama yule angependa kutoka naye kimapenzi?

“Ukiwa katika hilo, ningependa kuwaulizeni swali jepesi, kama yeye [mwanamke] angekuwa tajiri na we na vigezo sawia, unafikiri utakuwa chaguo lake?”

View Comments