In Summary

•Raquel na Mary Kirika walitumia bango kufikisha ujumbe wao kwa kijana huyo mrefu wakisema wanajitoa kwake.

•"Baraka zinakuja double double. Ninashukuru Wakenya kwa kuniunga mkono, nawapenda pia," Bradley alijibu.

Image: HISANI

Wanawake wawili warembo wanaodai kuwa dada kutoka kaunti ya Nakuru wamekiri mapenzi yao yasiyoisha kwa kijana Bradley Marongo almaarufu GenZ Goliath.

Raquel Kirika na Mary Kirika kama walivyojitambulisha, walitumia bango kufikisha ujumbe wao kwa kijana huyo mrefu wakisema wanajitoa kwake.

Kulingana na wao, Bradley anastahili wanawake wawili warembo na wameweka wazi kuwa wako tayari kuishi maisha yao yote naye.

"Sisi ni dada kutoka Nakuru, Raquel na Mary Kirika. Tuliketi na kuamua kijana mrefu na mwenye sura nzuri anastahili wanawake wawili warembo kando yako kukaa nawe maisha yako yote," wawili hao walisema kwenye bango hilo ambalo walishikilia.

Waliambatanisha ujumbe wao na namba zao za simu ili Bradley awafikie.

Kweli, kijana huyo mrefu alipata ujumbe huo na akatoa shukrani zake juu ya upendo ambao ameendelea kupata.

"Baraka zinakuja double double. Ninashukuru Wakenya kwa kuniunga mkono, nawapenda pia," Bradley alijibu.

Bradley ambaye amepewa jina la 'Gen-z Goliath alikuja kujulikana wakati wa maandamano ya kupinga serikali na ameendelea kupata umaarufu siku baada ya siku.

Kijana huyo tangu nyota ya jaha kumuangazia miezi miwili iliyopita wakati wa maandamano ya vijana wa Gen Z, amekuwa akipokea zawadi ainati, zingine zikiwa ni ahadi kutoka kwa watu mbalimbali.

Hivi majuzi, Mkurugenzi wa Bonfire Adventures, Simon Kabu baada ya kumfanikishia ziara ya siku chache kuelekea Pwani, alifichua kwamba kuna mtu kutoka taifa la Serbia ambaye amejitolea kumpa kijana huyo kazi nchini humo.

Pia, Bradley anasemekana kulamba dili nono la kuwa balozi wa mauzo katika chapa ya kampuni moja ya humu nchini ya kutengeneza unga.

View Comments