In Summary

•Diamond alikiri kuwa alijua kile ambacho wakosoaji walikuwa wakisema kwenye mitandao ya kijamii na aliamua kupuuza yote.

•Diamond alishikilia kuwa anamheshimu P Diddy kama msanii maarufu na hangeshughulikia tuhuma zozote zilizotolewa dhidi yake.

Image: hisani,

Staa wa Bongo Diamond Platnumz, hatimaye amevunja ukimya kuhusu tuhuma zinazoendelea mitandaoni kufuatia video ya zamani ikimuonyesha akiongea na gwiji wa muziki na biashara kutoka Marekani, P Diddy.

Baba huyo wa watoto 4 alikiri kuwa alijua kile ambacho wakosoaji walikuwa wakisema kwenye mitandao ya kijamii na aliamua kupuuza yote, akidumisha ana heshima kubwa kwa Sean Diddy Combs linapokuja suala la uwezo wake wa muziki.

"Mimi ni mtu ambaye huongelewa kwa maneno na kwa vitu tofauti... Maisha yangu mtandaoni, kwenye sanaa na kiuhalisia ni vitu tofauti sana. ...huwa sijibu maoni ya watu," alianza kwa mbali mwimbaji huyo wa 'Komasava' alipokuwa akihojiwa na chombo chake cha habari, Wasafi.

Aliendelea kujipiga kifua, akibainisha kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii bora sana katika tasnia ya muziki hivyo hakujali ni hadithi zipi zinazorushwa juu yake.

"Mimi ni miongoni mwa wasanii komavu na shupavu. Wewe andika na sema chochote unachotaka lakini sikujibu, sikohoi na sitetereki," aliongeza.

Huku akimalizia, Diamond alishikilia kuwa anamheshimu P Diddy kama msanii maarufu na hangeshughulikia tuhuma zozote zilizotolewa dhidi ya baba huyo wa watoto 11 mwenye umri wa miaka 54 hadi uamuzi utakapotolewa na mahakama za Marekani.

"Sitajifanya mchambuzi katika tukio lake kwa maana sijafanya sheria. Kwa ufupi, mpaka mahakama yaseme neno. Binafsi siwezi nikamhukumu lakini ninamheshimu kama mtu amvmbaye anajua vitu vingi vingi,"

Diddy kwa sasa anazuiliwa bila dhamana akisubiri kesi yake kufuatia mashtaka ya ulanguzi wa binadamu na ngono, ulaghai na unyanyasaji katika kitengo maalum cha makazi katika gereza la Metropolitan Detention Center.

View Comments