In Summary

•Keranta alipoulizwa ikiwa alim’cheat mpenzi huyo wake wa zamani, Keranta alionekana kukanusha ufahamu wa jambo kama hilo.

•Pia alikanusha kuwahi kunyanyashwa na mchekeshaji huyo, lakini akadokeza kuhusu mateso ya kiakili walipokuwa kwenye uhusiano.

Flaqo na aliyekuwa mpenzi wake Keranta
Image: HISANI

Aliyekuwa mpenzi wa Flaqo Raz Winnie Keranta hatimaye amevunja kimya kuhusu kutengana kwake na mchekeshaji huyo wa mitandaoni.

Katika kipindi cha moja kwa moja na shangazi ya Flaqo Nyakwar Janeko kwenye mtandao wa Tiktok, mtayarishaji huyo wa maudhui mwenye umri wa miaka 23 pia alizungumzia madai kwamba alikosa uaminifu katika mahusiano yake na mcheshaji huyo.

Keranta alipoulizwa ikiwa alim’cheat mpenzi huyowake wa zamani, Keranta alionekana kukanusha ufahamu wa jambo kama hilo.

“Mimi hiyo sijui. Enda uulize huyo mtu. Muende mtafute (uvumi) pia wa mtoto wenu,” Keranta alimwambia Bi Nyakwar.

Mtayarishaji wa maudhui huyo pia alionekana kuashiria kuwa hakuwa tayari kuwa na mtoto katika uhusiano wake wa miaka mitatu na Flaqo.

“Sasa kama sikuwa nataka.. miaka tatubila mtoto ata ni kidogo, ata ingefika tano,” alisema.

Pia alikanusha kuwahi kunyanyashwa na mchekeshaji huyo, lakini akadokeza kuhusu mateso ya kiakili walipokuwa kwenye uhusiano.

Akizungumzia gari alilozawadiwa na Flaqo katika siku yake ya kuzaliwa, alithibitisha kuwa mchekeshaji huyo ndiye aliye nalo kwa sasa.

Keranta aliweka wazi kuwa kwa sasa hayuko kwenye uhusiano wowote. Zaidi, alibainisha kuwa anafurahi na hali yake mpya ya uhusiano.

Flaqo na Keranta waliachana mapema mwaka huu. Wawili hao walikuwa pamoja kwa takriban miaka mitatu.

View Comments