In Summary

•Akothee alisema ni jambo zuri kupoteza ujauzito huo wa ambaye angekuwa mtoto wake wa kwanza na Denis ‘Omosh’ Schweizer.

•Mwanzoni, alionekana kujuta kwa nini hakungoja uhusiano wake na Bw Schweizer ukae kwa muda kidogo kabla ya kumpa ujauzito.

Akothee na aliyekuwa mume wake, Omosh
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwanamuziki na mjasiriamali maarufu wa Kenya Esther Akoth almaarufu Akothee amebainisha hadharani kwamba hajutii kamwe kupoteza ujauzito wake mwishoni mwa mwaka jana.

Akizungumza wakati wa kipindi cha moja kwa moja kwenye mitandao ya kijamii siku ya Jumanne jioni, mama huyo wa watoto watano alisema ni jambo zuri kupoteza ujauzito huo wa ambaye angekuwa mtoto wake wa kwanza na aliyekuwa mume wake, Denis ‘Omosh’ Schweizer.

Alisema kuwa kama hangepoteza ujauzito na badala yake ajifungue, hajui mambo yangekuwaje sasa kuona kwamba ndoa yake tayari imevunjika.

“Ata afadhali vile ile mimba ilitoka. Ile mimba kama ningezaa, uui!! Kama ningezaa ile mimba, saa hii sijui ningekuwa mgeni wa nani. Wewe unaona kama ningekuwa mgeni wa nani kama ile mimba ningezaa? Kama ningezaa ile mimba, ningekuwa mgeni wa nani na miaka 40? Naanza kukimbizana na mtu nikiwa na miaka 40?” Akothee alisema.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 43 alionekana kumsifu Mungu kwa ujauzito wake uliopotea na akabainisha kwamba ikiwa angejifungua, ingekuwa wakati mgumu sana kwake kushughulika na ambaye angekuwa mzazi mwenzake.

“Lakini huyu Mungu saa zingine ako na jokes zingine. Aliamua tu siku moja, asubuhi tu akasema hii haiwezi kitu kaa hapa akatoa akatupa huko. Saa hii ingekuwa kesi ingine, ningetoa huyo mtu kwa ngozi yangu namna gani,” alisema.

Mwanzoni, Akothee alionekana kujuta kwa nini hakungoja uhusiano wake na Bw Schweizer ukae kwa muda kidogo kabla ya kumpa ujauzito.

Hata hivyo aliweka wazi kuwa alikuwa tayari kuzaa alipokutana na mzungu huyo kutoka Uswizi na hata alikuwa kuenda Ulaya kununua mtoto.

"Jambo nililojifunza, sisi wanawake wakati mwingine sisi sio halisi kwa nafsi zetu. Sasa mbona sikukaa kidogo kwanza kabla hiyo?” Akothee alisema

Aliongeza, "(Omosh) Alipokuja maishani mwangu, nilikuwa tayari kupata mtoto. Nilikuwa tayari kabisa kwa mtoto, na ndio maana kufikia wakati Omosh anakutana na mimi, nilikuwa nimeenda Ualaya kununua mtoto, kwa sababu niko na pesa. Alipokuja alipata kama niko tayari, sio ati nilikuwa mjinga. Nilikuwa niko tayari kuzaa, lakini sasa kangekuwa hapa hivi na tum+tak+ kidogo kama baba yake anazunguka zunguka kwa huu uwanja. Ningekuwa sasa mtoto namba ngapi?

Wakati huo huo, mwimbaji huyo ambaye maisha yake yamezungukwa na drama nyingi aliweka wazi kuwa ndoa yake ya muda mfupi na Omosh iligonga mwamba mwezi Juni. Alisema wakati walipokuwa kwenye fungate baada ya harusi yao mwezi Aprili alijifunza mambo ambayo hangeweza kustahimili.

View Comments