In Summary

•Mama huyo wa watoto watano aliwaonya wanadada dhidi ya kuingia katika mahusiano na wanaume ambao tayari wana familia.

•Akothee aliweka wazi kuwa ni sheria yake kutochumbiana na mwanamume ambaye ana mke hata awe katika hali gani.

Image: FACEBOOK// AKOTHEE

Mwimbaji na mjasiriamali maarufu wa Kenya Esther Akoth almaarufu Akothee ameweka wazi kuwa kamwe hawezi kuchumbiana na mwanamume ambaye ana mke.

Katika taarifa ya Jumapili, mama huyo wa watoto watano aliwaonya wanadada dhidi ya kuingia katika uhusiano na wanaume ambao tayari wana familia.

Alishangaa kwa nini wanawake wadogo wanachagua kujitosa kwenye mahusiano na wanaume ambao hawana mpango wa kuwaoa kwani wana familia.

"Wasichana wadogo, mnatamani nini kwa mwanamume aliyeoa na ana watoto? Hebu fikiria, hata kwa mahusiano yangu yote ambayo yamefeli, siwezi kuridhika na mwanaume aliyeoa, na haswa yule ambaye hawezi kukidhi matarajio yangu kama msichana 🤔 Ahhh, kwa hivyo una mpango gani wa mchezo?" Akothee alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Aliongeza, “Wewe tayari umekubali kuwa mpango wa kando, pengine wazazi wako walitumia gharama kubwa kukusomesha ili uwe na maisha marefu ya baadae. Alafu unaruhusu mwanaume aliyeoa aje kukutongoza kwa upuuzi usio na maana , akutumie kukata Kiu yake ya tendo la ndoa 🤔 utakuwa na nini kimebaki wakati unataka kutulia ? Je, yuko tayari kutulia na wewe, ama anakula asonge mbelee?

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 43 alishangaa jinsi wanawake wanaojihusisha na wanaume walioolewa wanahisi wakati wapenzi wanadanganya wake na watoto wao.

“Amekutambulisha kwa mkewe na watoto wake? mke wake yuko sawa? Familia yake? Unajisikiaje anapokaa nawe siku na usiku wake wote, akim’cheat mkewe na watoto wake kwamba yuko kazini kufunga dili, je wewe ni WAJIBU? Au mambo yako ni DILI YENYEWE?" aliandika.

Mwimbaji huyo alibainisha kuwa ni sheria yake kutochumbiana na mwanamume ambaye ana mke hata awe katika hali gani.

“Niangalie mimi nina miaka 40 na mwanaume aliyeoa ni HAPANA, imekuwa ni Kanuni yangu siku zote. Vitu vyote vilivyo chini ya kitanda vitatolewa hivi karibuni na PANYA 🐀. Endelea kukusanya laana kutoka kwa machozi ya wale wanawake walioachwa na waume zao. Hata wewe ipo siku utakaa chini. Mpaka asubuhi ukingoja mumeo arudi nyumbani,” alisema.

Aliongeza, “Najua sifai kumshauri mtu yeyote kuhusu mahusiano, kwani yangu yalifeli mara kadhaa. LAKINI UKWELI UWE UKWELI. WANAUME WALIOOA WAKAE NA WAKE ZAO. WACHENI WASICHANA WAJITAFUTIE MAISHA. Eeee, ,Mwanaume aliyeoa, Labda aninunulie feri.”

View Comments