In Summary

•Akothee alionekana kutupilia mbali mawazo kuwa yeye ndiye aliondoka na akasema mengi mazuri kuhusu mpenziwe huyo.

•Akothee alisisitiza kuhusu harusi kubwa sana inayokuja ambapo atakuwa akifunga pingu za maisha na mpenzi huyo.

Akothee
Image: HISANI

Mwimbaji Esther Akoth almaarufu Akothee alikuwa kwenye mahojiano hivi majuzi ambapo alizungumzia masuala mbalimbali kuhusu maisha yake ambayo hufuatiliwa sana.

Katika mahojiano hayo, moja ya maswali magumu ambayo alikabiliwa nayo ni kuhusu kwa nini aliachana na mpenzi wake Nelly Oaks na kuolewa na Denis Schweizer almaarufu Omosh.

Msanii huyo katika majibu yake hata hivyo alionekana kutupilia mbali mawazo kuwa yeye ndiye alikuwa ameondoka na akasema mengi mazuri kuhusu mpenziwe ambaye pia ni meneja wake.

“Watu wanafikiri kwamba nilimwacha. Nelly ni mtu mtanashati. Kwa nini unadhani mimi ndiye niliyemuacha. Kwa sisi watu mashuhuri, hatuweki kila kitu kwenye kamera,” Akothee aliambia gazeti la The Nairobian.

Mama huyo wa watoto watano aliendelea kufunguka kuhusu jinsi Nelly Oaks alivyomsaidia na kusimama naye mara nyingi ikiwa ni pamoja na baada ya kuvunjika kwa ndoa yake na Omosh mwaka jana.

“Amekuwepo kwa ajili yangu. Yeye ndiye mtu aliyeunda chapa hii na kuniona nikipitia hali ya msongo wa mawazo mara tatu kati ya nne. Alinitembeza kupitia kutengana. Alinitunza,” alisema.

Katika mahojiano hayo, mwimbaji huyo alisisitiza kuhusu harusi kubwa sana inayokuja ambapo atakuwa akifunga pingu za maisha na mpenzi huyo ambaye pia ni meneja wake.

Alibainisha kuwa harusi aliyofanya na Omosh Aprili mwaka jana ilikuwa ya mazoezi tu na akadokeza kuwa harusi yake ijayo na Nelly Oaks itakuwa bora zaidi.

“Yalikuwa mazoezi, harusi inakuja sasa hivi naenda kuolewa na mwanaume wa ndoto zangu. Niko kwenye uhusiano thabiti kwa sasa lakini pia nahitaji nafasi ya kukatishwa tamaa kwa sababu wana wa Farao wanaweza kukuonyesha mavumbi,” alisema.

Katika siku za hivi majuzi, Akothee amekuwa akidokeza sana kuhusu harusi kubwa inayokuja ambapo anatarajiwa kufunga ndoa rasmi na Nelly Oaks.

Akothee na Nelly Oaks wamekuwa wakisherehekea mapenzi yao waziwazi katika miezi kadhaa iliyopita, baada ya kurudiana tena kufuatia kuvunjika kwa ndoa ya Akothee na ex wake Denis Schweizer katikati mwa mwaka uliopita.

Mwishoni mwa mwaka jana, mwanamuziki huyo  alionekana kuthibitisha kufufuka kwa mahusiano yake na Nelly Oaks katika kipindi cha moja kwa moja kwenye mtandao wa TikTok.

Katika kipindi hicho, Akothee alisikika akimwita meneja huyo wake ‘babe’ mara kadhaa, jina ambalo hutumika sana sana  wapenzi.

Nelly Oaks pia alisikika akimtaja Akothee kama mtu maalum kwake huku wawili hao wakishiriki matukio ya kimapenzi kwenye kamera.

View Comments