In Summary

• Shabiki alimtaka Akothee atoe tamko kuhusu kile kilichotokea kwa kile kilichoonekana kama muungano mzuri.

•"Biashara ni muhimu kwako kuliko uhusiano wangu, jifunze kutoka kwangu wachana na uhusiano tafadhali kabla sijakublock, hiyo ni ya faragha." Akothee alisema.

Akothee na mkewe Denis Shweizer
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Katika kipindi cha miezi michache iliyopita, watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakiibua wasiwasi mwingi kuhusu hatima ya ndoa ya mwimbaji na mjasiriamali mashuhuri wa Kenya Esther Akoth almaarufu Akothee na mzungu Denis Shweizer almaarufu Bw Omosh.

Akothee alifunga ndoa na mzungu huyo kutoka Uswizi katika harusi ya kifahari iliyofanyika jijini Nairobi mnamo Aprili 10, mwaka huu. Baada ya harusi hiyo iliyohudhuriwa na wanafamilia, marafiki na watu wengine mashuhuri, wapenzi hao walikaa pamoja kwa muda na waliendelea kuwapasha mashabiki wao kuhusu mahali walipo pamoja kabla ya polepole kuacha kuonekana wakiwa pamoja au hata kusherehekeana kama walivyokuwa wakifanya awali. Hatua hii limewaacha wengi na maswali mengi yasiyo na majibu, jambo ambalo limefanya wapige hatua ya kutafuta majibu kutoka kwake.

Chini ya moja ya machapisho ya mitandao ya kijamii ya mwimbaji huyo, mwanamtandao mwenye wasiwasi alimtaka atoe tamko kuhusu kile kilichotokea kwa kile kilichoonekana kama muungano mzuri.

“Unaweza kutuambia kitu kuhusu Omosh? Unamaanisha kuwa Omosh anafifia kutoka kwenye nyuso zetu.. tafadhali isiwe..,” Daktari Dalton Milalu alitoa maoni kwenye Facebook.

Mama huyo wa watoto watano kwa ujasiri alijibu, "Biashara ni muhimu kwako kuliko uhusiano wangu, jifunze kutoka kwangu wachana na uhusiano tafadhali kabla sijakublock, hiyo ni ya faragha."

Mwanamitandao mwingine pia alibainisha kuwa ni muda mrefu tangu Akothee alipomuonyesha mzungu huyo au hata kumzungumzia na kumuuliza ikiwa harusi ya pili bado ipo.

"Omosh anafifia na upepo..#luo gods hawajakaa ..#oyugi na akoth Harusi ya kweli inakuja ..#tafadhali usinitusi  naomba," Dan Lucas Fitzben alisema.

Akothee akajibu, “🤣🤣🤣🤣 idhi ketho gini" (Unaenda neno hili kitu).

Akothee na Shweizer walifunga pingu za maisha katika harusi ya kufana iliyoandaliwa katika hoteli ya Windsor Golf Hotel, Kiambu Road mnamo Aprili 10 kabla ya mzungu huyo kuelekea Uswizi siku chache baadaye kwa sababu za kikazi.

Mama huyo wa watoto watano baadaye alitembelea Bw Shweizer nchini Uswizi mwezi Juni kabla ya kurejea humu Kenya na hiyo ndiyo mara ya mwisho wanandoa hao walionekana wakiwa pamoja.

View Comments