In Summary

•Bahati ambaye alionekana waziwazi kutokuwa na wasiwasi alichapisha video ya familia yake na kujigamba jinsi walivyo mada ya habari.

•Miongoni mwa mambo ambayo wanamitandao walishambulia familia ya Bahati  kuhusu ni mtindo wa mavazi ya Diana Marua

Familia ya Bahati
Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Mwanamuziki Kelvin Kioko almaarufu Bahati amejibu kwa njia isiyo ya moja kwa moja baada ya wanamitandao wa Kenya kugeuza familia yake kuwa mada ya mjadala wa kitaifa katika siku chache zilizopita.

Wikendi na sehemu kubwa ya siku ya Jumatatu, mwimbaji huyo wa zamani wa nyimbo za injili, mkewe Diana Marua na familia yao yote walikuwa wakivuma kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ambako wanamitandao walijadili masuala mbalimbali kuhusu maisha yao.

Katika taarifa fupi mnamo Jumatatu jioni, Bahati ambaye alionekana waziwazi kutokuwa na wasiwasi alichapisha video ya familia yake na kujigamba jinsi walivyo mada ya habari.

"Sisi ni familia ya Bahati. Sisi ndio Watengenezaji wa Habari!!! Leo wanasemaje??" Bahati alisema chini ya video aliyochapisha kwenye mtandao wa Instagram.

Video ambayo mwanamuziki huyo alichapisha ilinasa nyakati zuri zake, mkewe na watoto wao katika nyumba yao ya kifahari.

Miongoni mwa mambo ambayo wanamitandao walishambulia familia ya Bahati siku ya Jumapili na Jumatatu ni mtindo wa mavazi ya Diana Marua wakati wa kipindi cha picha ya familia. Baadhi ya Wakenya waliliona vazi ambalo mama huyo wa watoto watatu alivaa katika picha hizo kuwa halifai na kumkosoa kwa hilo.

Katika sehemu ya maoni ya chapisho lake la Jumapili ambapo alipakia picha yake na mwanawe Morgan Bahati, wanamitandao wengi hawakuonekana kuangazia maneno mazuri ambayo mke huyo wa Bahati alimwandikia mtoto huyo wake wa kulea bali waliangazia vazi alilovaa. Wengi wa wale waliotoa maoni walionekana kumshambulia kwa chaguo lake la mavazi huku baadhi wakimdhihaki.

Kundi la watumiaji wanamitandao ya kijamii waliotoa maoni yao walionekana kumshauri mama huyo wa watoto watatu kuwa makini na mavazi anayovaa mbele ya watoto wake, wengine walimkosoa, baadhi wakamtetea huku wengine wakidai kuwa suruali yake ya ndani ilionekana pichani.

Tazama baadhi ya maoni ya wanamitandao Wakenya:-

@escob3r:  Advise...... No hard feelings but truth be told you are are great mother but the dress code should change...... But kudos to your progress and keep being the good mother you are.

@evesheryk:  this is wrong...it is good for u bt embarrassing the boy to his peers .He cnt be proud to show such a pic to his peers coz her moms panty is visible.I am ua big fan n happy for ua wins bt hii sitakimya

@chelangat.bridgid: Diana b pliz wear clothes decent clothes for once.

Awour.00: your son is now grown.. wear decent clothes..ukweli nayo tutakua coz tunakupenda

i_am_njeri_whit: Can't you dress/ wear decently Infront of your kids

winfaithfulofficial: Siungevaa kitenge hata jamani mngetokea supuu Sana Infront of a teenager son

View Comments