In Summary

•Betty ambaye ameapa kumficha mpenzi wake wa sasa hata hivyo amedokeza kuwa atamsherehekea chini ya maji.

•Betty  alianza kudokeza kwamba amezama kwenye mahusiano mapya takriban miezi mitatu iliyopita.

Image: INSTAGRAM// BETTY KYALLO

Mtangazaji maarufu Betty Kyallo amedokeza kuwa mpenzi wake asiyejulikana anaadhimisha siku ya kuzaliwa hivi leo, Februari 2.

Betty ambaye ameapa kumficha mpenzi wake wa sasa hata hivyo amedokeza kwamba atamsherehekea chini ya maji.

"Kwa  wale wanasema Valentines ni kila siku, leo umepewa maua na nani?? Alafu leo ni siku ya kuzaliwa ya mtu, chini ya maji❤❤," alisema kwenye video yake ambayo alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kwenye Instastori, mama huyo wa binti mmoja pia alimtakia heri ya sikuy ya kuzaliwa mpenzi huyo wake.

"Kheri ya siku ya kuzaliwa mpenzi wangu,"  aliandika.

Betty Kyallo alianza kudokeza kwamba amezama kwenye mahusiano mapya takriban miezi mitatu iliyopita.

Mwezi Oktoba, alichapisha picha yake akiwa ameshikilia shada la maua, na kusema hilo ndilo tukio maalum la wiki yake.

"Mapenzi ni kitu kizuri," aliandika.

Takriban wiki tatu zilizopita, Betty alifichua kuwa ana mwanamume ambaye wanachumbiana naye mwaka huu wa 2023.

Betty katika mahojiano kwa njia ya simu na kituo kimoja cha redio humu nchini alisema kuwa hawezi kaa peke yake huku akikataa kabisa kumzungumzia mwanaume huyo wake na kusema hatoweka jina lake wazi.

Mtangazaji alimuuliza Betty kutoa maelezo zaidi na akasema kuwa “acha nikate simu kabla niachwe!”

Alisema kuwa watu hawawezi kumjua mpenzi wake kwa urahisi, akidokeza kuwa pengine wanaweza kuwa wanamuona bouncer akimpa ulinzi kumbe ndio mtu wake.

“Safari hii NAMFICHA kama bangi... Ni 2023....Labda ata ni Bodyguard wangu na Hamumjui.... " Kyallo alisema kwa utani.

Mahusiano ya mwisho ya hadharani ya mfanyibiashara huyo wa nywele yalikuwa na wakili Nick Ndeda.

Wawili hao walipoachana, Betty alisema walikuwa na mitazamo tofauti ya masuala fulani ya kimaisha.

"Katika mahusiano, ni kuhusu kufahamiana. Ilifika mahali ambapo tulikuwa hatuna mwelekeo sawa upande na uhusiano."

View Comments