In Summary

•Edday alichapisha ujumbe wa kutia moyo na kuuambatanisha na hashtagi kadhaa ambapo katika mojawapo alijiita Bi Nyandarua.

•Rafiki yake wa karibu, Bernice Saroni alithibitisha nia yake ya kujitosa katika ulingo wa siasa.

Image: INSTAGRAM// EDDAY NDERITU

Bi Edday Nderitu, mke wa mwimbaji wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh amedokeza kuwa atawania kiti cha ugavana wa kaunti ya Nyandarua katika siku za usoni.

Siku ya Alhamisi, mama huyo wa watoto watatu alichapisha ujumbe wa kutia moyo na kuuambatanisha na hashtagi kadhaa ambapo katika mojawapo alijiita Bi Nyandarua.

“Baada ya kuishi, jifundishe jinsi ya kustawi. Kwa sababu unastahili kuwa na furaha baada ya kufanikiwa kupitia kila kitu ambacho kilijaribu kukuangamiza. #nothingbutprayers #mrsnyandarua #eddaynderitu ,” Edday aliandika kwenye kurasa zake za mitandao ya Instagram na Facebook.

Aliambatanisha ujumbe huo na picha yake nzuri.

Hashtag ya #BiNyandarua ilizua mjadala kwenye sehemu ya maoni huku baadhi ya mashabiki wakimsukuma kufafanua alichomaanisha.

“Ati Mrs nini?,” mtumiaji mmoja wa Instagram alimuuliza.

Huku akimjibu shabiki huyo, Edday alisema, "Future gavana wa Nyandarua."

Rafiki yake wa karibu, Bernice Saroni alithibitisha nia yake ya kujitosa katika ulingo wa siasa huku akimuita kama gavana wa baadaye wa kaunti hiyo ya eneo la Mlima Kenya.

“Gavana wetu wa baadaye wa Nyandarua. Nakupenda siz,” aliandika Bernice chini ya chapisho la Edday.

Edday hata hivyo hakufichua maelezo zaidi kuhusu azma yake ya kisiasa na hakuweka wazi ni lini anapanga kuwania kiti hicho  cha juu zaidi cha kaunti.

Baadhi ya wafuasi wake walimtakia heri katika azma yake ya kisiasa. Baadhi hata hivyo walionekana kukejeli tangazo lake. Soma baadhi ya maoni yake hapa chini;

Perisita4: Watu wa Nyandarua tume approve. Keep keeping on mama. Ngapi mbele

Moniqa_mungai: Mrs Nyandarua it is. I really want the best for you Edday. May God hear our prayers, I wish you more peace and grace to thrive.

N_yambura Sisi tunataka ukae US. Mambo ya Nyandarua/Kenya aachia wengine

Salimamureithi wuee, ati mrs nyandarua… anyway you look good maa

Suziedarsh Thrive Mrs Nyandarua.

Je, ushauri wako ni upi kwa Bi Edday Nderitu anapojitosa katika siasa?

View Comments