In Summary

•Diana simulia jinsi Morgan alivyokuwa akimuita shangazi yake katika siku zake za kwanza na Bahati hadi ilipofika wakati akaomba kumuita mama.

•Diana alibainisha kuwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 14 amekuwa baraka kubwa katika maisha yao na kumshukuru Mungu kwa kumleta kwao.

Diana Marua na Morgan Bahati.
Image: Insta

Siku ya Ijumaa, mwanavlogu maarufu wa YouTube Diana Marua alimsherehekea mumewe Kelvin ‘Bahati’ Kioko na mwanawe wa kulea Morgan Bahati katika siku yao ya kuzaliwa.

Bahati alifikisha umri wa miaka 31 mnamo Desemba 22, 2023 huku Morgan akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya 14 katika siku hiyo hiyo.

Wakati akiwasherehekea wanaume hao wawili maalum katika maisha yake kupitia mitandao ya kijamii, Diana alitoa historia fupi yake na Morgan akifichua jinsi kijana huyo alivyokuja  kuwa sehemu ya maisha yake.

“22/ 12/ 2023 MWANANGU @MORGANBAHATI  ANATIMIZA MIAKA 14 NA MUME Wangu BAHATI  AKITIMIZA MIAKA 31 ������������,” Diana Marua aliandika kwenye Instagram.

Mwanavlogu huyo aliendelea kusimulia jinsi Morgan alivyokuwa akimwita shangazi yake katika siku zake za kwanza na Bahati hadi ilipofika wakati kijana huyo akaomba kumuita mama yake.

"Nilipokutana na mume wangu, alikuwa amemchukua Morgan kutoka kwenye nyumba ya watoto ambayo wote walikuwa wamelelewa. Nilimpenda Bahati kwa kila kitu kilichokuwa ndani yangu pamoja na kila mtu aliyemzunguka. Morgan alizoea kuniita Aunty Dee na miezi michache baadaye, aliniambia… Je, naweza kukuita Mama? kwa sababu marafiki zangu wanauliza kwa nini niwaite Baba, Baba na wewe Shangazi na wanakuona pamoja… watoto hawa ingawa IFYYK,” alisema Diana Marua.

Aliongeza, “Nilimuuliza, utakuwa sawa kuniita Mama, akasema… ndivyo ninavyotaka. Nilimiliki jina la Mama kwa mara ya kwanza, miaka 7 iliyopita kupitia Morgan .”

Mama huyo wa watoto watatu alibainisha kuwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 14 amekuwa baraka kubwa katika maisha yao na kumshukuru Mungu kwa kumleta kwao.

"Morgan, natumai umepata upendo ndani yetu, kwa sababu hatungewahi kuomba baraka Kubwa zaidi ya ile ya kuwa wazazi wako ❤️," Diana alimwandikia mwanawe mlezi.

Katika ujumbe wake mwingine kwa mwanawe, mke huyo wa Bahati alimtaka kijana huyo wa miaka 14 kukumbuka daima jinsi Mungu amewatoa mbali.

"Nakupenda Morgan Bahati," Diana aliandika.

Mama huyo wa watoto watatu pia alijivunia uamuzi wake wa kuwa sehemu ya maisha ya Bahati na mwanawe akiutaja kuwa uamuzi bora zaidi kuwahi kufanya.

View Comments