In Summary

•Video inamuonyesha Shakib akisema viapo vya ndoa kisha kumvisha Zari pete kidoleni kabla ya wageni kupiga makofi kwa nguvu

•Wanawe Zari na aliyekuwa mume wake, Ivan Ssemwanga walionekana wamevalia suti nyeupe, shati jeupe na viatu vyeupe.

Zari na Shakib walifunga ndoa Oktoba 3, 2023.
Image: HISANI

Sasa ni rasmi kwamba wapenzi maarufu wa Uganda, Zarinah Hassan na Shakib Cham Lutaaya ni mke na mume.

Wawili hao walifunga pingu za maisha katika harusi nzuri ya faragha ambayo ilifanyika siku ya Jumanne katika eneo lisilobainishwa nchini Afrika Kusini, ambapo wote wanaishi. Wamekuwa wakichumbiana kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Maelezo ya harusi hiyo yalikuwa yamefichwa sana lakini Radio Jambo imefanikiwa kupata baadhi ya picha na video za sherehe hiyo ya kukata na shoka.

Picha hizo zinaonyesha mwanasosholaiti Zari Hassan akiwa amevalia gauni la harusi refu jeupe huku mumewe Shakib akiwa amevalia suti ya kijivu na shati jeupe.

Wanafamilia wakiwemo watoto wa Zari; ; Pinto Tale, George Ssemwanga, Dido Ssemwanga Tiffah Dangote na Prince Nillan walikuwepo kwenye hafla hiyo. Tiffah alivalia gauni jeupe huku Nillan akiwa amevalia suti ya kijivu na shati jeupe sawa na bi na bwana harusi.

Wanawe Zari na aliyekuwa mume wake, Ivan Ssemwanga walionekana wamevalia suti nyeupe, shati jeupe na viatu vyeupe.

Wengi wa wageni waliokuwa wamealikwa kuhudhuria hafla hiyo ya faragha walionekana wamevaa mavazi meupe. Wanaume walikuwa na suti ya kijivu wakati wanawake walivaa gauni za rangi ya dhahabu.

Video inamuonyesha Shakib akisema viapo vya ndoa kisha kumvisha Zari pete kidoleni kabla ya wageni kupiga makofi kwa nguvu. Video nyingine inawaonyesha wanandoa hao wakiwa na watoto wa Zari wakipigwa picha ya familia huku wageni wakipiga makofi.

Mama yake Shakib pia alikuwepo kwenye sherehe hiyo.

Sherehe hiyo ilirekodiwa na watengeneza filamu ya Netflix ya Young, Famous and African na itaonyeshwa katika msimu ujao.

Harusi hiyo ilifanyika Afrika Kusini na ilihudhuriwa na wageni wachache tu walioalikwa.Maelezo mengi kuihusu yaLIwekwa faragha. Haijabainika kwanini wapendanao hao waLIweka harusi yao kuwa siri kubwa.

Wawili hao walihalalisha muungano wao wa muda mrefu kwa mara ya kwanza katika harusi ya kidini ya Kiislamu (Nikah) mapema mwaka huu.

Walifunga ndoa ya Kiislamu mwezi Aprili baada ya kuwa wamechumbiana kwa takriban mwaka mmoja. Walivishana pete katika hafla ya faraghani ambayo ilihudhuriwa na idadi ndogo ya watu wakiwemo wanafamilia na marafiki.

View Comments