In Summary

•Nyamu alibadilisha picha yake ya wasifu kwenye mtandao wa Instagram na kuweka picha inayomuonyesha akiwa na mzazi huyo mwenzake pamoja na binti yao mdogo.

•umatano usiku, alionyesha picha kadhaa za yeye, Samidoh na mtoto wao wa mwisho  na kuambatanisha na wimbb 'Foto Moto'

Karen Nyamu na Samidoh
Image: HISANI

Ni wazi kwamba seneta wa kuteuliwa Karen Nyamu amezama kabisa kwenye dimbwi la mahaba na mwimbaji Samuel Muchoki almaarufu Samidoh.

Siku ya Ijumaa, mama huyo wa watoto watatu alichukua hatua kubwa ya kubadilisha picha yake ya wasifu kwenye mtandao wa Instagram na kuweka picha inayomuonyesha akiwa na mzazi huyo mwenzake pamoja na binti yao mdogo.

Nyamu alitumia moja ya picha  walizopigwa wakati wa kusherehekea siku ya kuzaliwa ya binti yao Wairimu mwezi Februari mwaka huu.

Image: INSTAGRAM// KAREN NYAMU

Haya yanajiri siku mbili tu baada ya mwasheria huyo aliyezingirwa na drama si haba kuonyesha picha kadhaa za karamu ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya bintiye iliyofanyika Februari ambazo hakuwahi kuonyesha hapo awali.

Siku ya Jumatano usiku, alionyesha picha kadhaa za yeye, Samidoh na mtoto wao wa mwisho  na kuambatanisha na wimbb 'Foto Moto'

Mapema wiki hii, seneta huyo wa kuteuliwa alizua gumzo baada ya kutumia picha zingine zake, mzazi mwenzake na binti yao  kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa mtoto wa Samidoh pamoja na Edday Nderitu kwa njia ya kikejeli.

“Sawa kutokana na madai ya umma hehehe. Baba mzuri anastahili watoto wengi. Heri ya kuzaliwa Neriah Muchoki,” aliandika.

Hatua ya Nyamu ilifuata baada ya Bi Edday kuonyesha picha nzuri za karamu ya siku ya kuzaliwa ya binti yake Neriah Wairimu.

 Edday alibainisha kwamba karamu hiyo iliyohudhuriwa na wanafamilia pamoja na marafiki wa karibu wa familia ilikuwa ya kusisimua.

"Sherehe ya kupendeza ilikuwa, asante familia na marafiki kwa kujumuika nasi kusherehekea siku ya kuzaliwa ya binti yangu ya kwanza, sherehe ilipamba moto, nguvu ilikuwa katika kiwango kingine," alisema kwenye Facebook.

Mkewe Samidoh alionyesha picha kadhaa za karamu hiyo ya kukata na shoka ambayo ilifanyika nyumbani kwao. Pichani, yeye, mumewe na watoto wao watatu walionekana wenye furaha tele pamoja.

Video zilizochukuliwa wakati wa karama hiyo zilionyesha wazazi wenza hao wawili wakicheza densi na kuburudisha wageni pamoja.

Huku wakidensi kwa wimbo wa hivi majuzi wa Samidoh na Prince Indah 'Bado Nakupenda', wanandoa hao walionekana wakikumbatiana kwa mahaba huku wakinengua viuno kwa mitindo ya kimapenzi.

View Comments