In Summary

•Marioo alionekana akimkabidhi Paula noti za pesa za Tanzania huku akibainisha kuwa hiyo ndio njia yake ya kutongoza.

•Marioo alifichua kwamba alikuwa bikra wakati alipoachia wimbo wake wa kwanza  mwaka wa 2017.

Marioo na Paula
Image: INSTAGRAM// MARIOO

Mwimbaji wa Bongo Omary Mwanga almaarufu Marioo na mwanamitindo Paula Paul Kajala wameendelea kuonyesha mahaba mazito baina yao.

Siku ya Alhamisi, binti huyo wa muigizaji Frida Kajala Masanja alichapisha video yake akifurahia muda na mwimbaji huyo wa kibao 'Mi Amor.'

"Sugar daddy wangu," Paula aliandika kwenye video hiyo ambayo alichapisha kwenye akaunti yake ya mtandao wa Snapchat.

Kwenye video hiyo, wawili hao walionekana kuwa na wakati mzuri pamoja ndani ya chumba cha kulala. Marioo alivaa vesti na kaptura ilhali  Paula hakuonekana vizuri kwani yeye ndiye aliyekuwa akirekodi video hiyo.

Mwimbaji huyo alionekana akimkabidhi Paula noti za pesa za Tanzania huku akibainisha kuwa hiyo ndio njia yake ya kutongoza.

"Mwenzenu mimi sijui kutongoza, ukijipitisha. Namwaga hela," alisema huku Paula akicheka nyuma ya kamera aliyoshika.

Akizungumza kwenye mahojiano na Millard Ayo, mwanamuziki huyo alikiri kuwa alipata mpenzi wa kwanza baada ya kujitosa kwenye usanii.

Marioo alifichua kwamba alikuwa bikra wakati alipoachia wimbo wake wa kwanza  mwaka wa 2017.

"Nashukuru Mungu nimeingia kwenye game mapema. Naweza  kusema nimeingia kwenye game nikiwa bikira, sijakutana na mwanamke," alisema.

Alisema kwamba hakuna chochote kilichokuwa kinamzuia kupata mpenzi lakini hakuwa tayari kwa mahusiano. Alisema alipata mwanamke wake wa kwanza akiwa anaishi na kaka yake lakini mpenzi huyo alimtema baadaye.

Katika siku kadhaa za hivi majuzi, Marioo amekuwa akionekana akijivinjari na mwanamitindo mrembo wa Bongo, Paula Kajala.

Haijabainika iwapo wawili hao wanatoka kimapenzi lakini kwa hakika wamekiri kupendana. Siku chache zilizopita, Marioo alisifu urembo wa mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 20 na kubainisha kuwa anampenda.

"Imagine mtoto mbichi kama huyu alafu anakupenda.. @therealpaulahkajala #ananipenda inakuja hivi karibuni," Marioo aliandika chini ya video ya Tiktok ya Paula akicheza wimbo wake mpya 'Ananipenda.' 

Huku akijibu kwenye chapisho hilo la Instagram, binti huyo wa muigizaji Kajala Masanja alisema laiti wangekutana awali.

"Natamani ningekutana nawe awali," aliandika na kuambatanisha na emoji zilizoashiria mahaba mazito kwake.

Marioo aliendelea kumtambua mwanamitindo huyo kama kipenzi chake.

View Comments