In Summary

•Baadhi ya wanamitandao hata walidai kuwa Karen Nyamu alipigwa na Samidoh, madai ambayo tayari ameyapuuzilia mbali.

•Edday ambaye kwa muda mrefu amekuwa kwenye mzozo mkali na seneta huyo wa UDA alijibu kwa kusema, "Hizo huwa kama prescription."

Seneta Karen Nyamu na Bi Edday Nderitu
Image: FACEBOOK

Bi Edday nderitu, mke wa Samidoh amechangia katika mjadala unaoendelea mitandaoni kuhusu madai tata kwamba mwimbaji huyo wa Mugithi alimshambulia mpenzi wake mwingine na mzazi mwenzake, Karen Nyamu.

Wikendi, picha ya seneta Karen Nyamu akiwa na uso wenye michubuko ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuzua uvumi kwamba alikuwa mwathiriwa wa dhuluma za nyumbani. Baadhi ya wanamitandao hata walidai kuwa seneta huyo alipigwa na mpenzi wake Samidoh, madai ambayo tayari ameyapuuzilia mbali.

Huku akijibu chapisho la Facebook la Edday Nderitu, shabiki mmoja alimkejeli seneta Nyamu kwa kumnunulia mzazi mwenzake kinywaji cha bei ghali kisha baadaye kudaiwa kupigwa.

“Kule kwingine ata baada ya kununua pombe ya 420 lakini malipo malipo ni mangumi. Hakuna ila maombi, " mtumiaji wa Facebook aliandika kwenye ukurasa wa Edday.

Edday ambaye kwa muda mrefu amekuwa kwenye mzozo mkali na seneta huyo wa UDA alijibu kwa kusema, "Hizo huwa kama prescription."

Hapo awali, seneta Karen Nyamu alikanusha madai ya dhuluma za nyumbani kufuatia wasiwasi mkubwa ulioibuliwa katika mitandao ya kijamii baada ya kuonekana hadharani akiwa na michibuko usoni.

Siku ya Jumatatu, kwenye mtandao wa Facebook, shabiki mmoja alimwandikia, “Walisema eti umechapwa na Samidoh.”

Nyamu ambaye anajulikana kuwa mbishi sana katika majibu yake kwa wanamitandao alisema kwa utani, "Na tarimbo."

Mtumiaji mwingine wa Facebook aliandika “Washow wewe labda uchapwo na Dickson Munene, my favourite.”

Alijibu, "Wanajifanya hawajui."

Siku ya Jumapili jioni, seneta Nyamu alikanusha tetesi za mitandaoni kwamba jicho lake jeusi lililoonekana kwenye picha iliyosambaa mitandaoni lilitokana na unyanyasaji wa kinyumbani.

"Mnajua mimi si mtu wa kujali wanachosema kuhusu maisha yangu binafsi au chochote kile. Chochote unachotaka kusema juu yangu unajua inakuanga bure. Sicatch, sijali kwani sina issue kabisa. Kwa kweli saa zile hamniongelei nakuangaa na wasiwasi kidogo."

Nyamu aliwahutubia wanamitandao katika kipindi cha moja kwa moja kwenye Facebook ambapo alijibu wasiwasi kuhusu jicho lake na kufunguka kuhusu changamoto anayokabiliana nayo.

"Lakini kuna jambo ambalo limenivutia. Ni picha ambayo tulipiga siku ya Ijumaa kwenye hafla moja huko Nyeri katika Ofisi ya Skauti na Girl Guides ambapo spika wa Seneti alikuwa mgeni mkuu katika hafla ya kufunga na hivyo tulikuwa tumeandamana na yeye na maseneta kadhaa na hii picha nimepigwa imefunika macho yangu moja, whatever alafu sijui kuna nini.

Kwa hiyo watu wanakejeli unyanyasaji wa kijinsia hasa watu wale hawanilike, wanafikiri ukatili wa kijinsia ni kitu ambacho unaweza kukitumia kujibu mzozo au kitu ambacho unapaswa kuwatakia maadui zako na hawa ni wanawake. Hatuwezi kuwa wajinga hivi katika zama hizi. Unyanyasaji wa kijinsia ni suala zito, unaathiri asilimia 40 ya wanawake nchini Kenya kama vile Afrika unavyoathiri wanawake zaidi kuliko wanaume,"  alisema.

Alisisitiza hakuna mtu aliyempiga, na hapakuwa na jicho jeusi.

View Comments