In Summary

• Majibu yake yaliwafurahisha wawili hao wa studio na Smriti akacheka, "Leila, wewe kweli ni shujaa wangu usiku wa leo," huku Mark akiangua kicheko.

Mwanahabari Leila Mohammed wa kituo cha runinga cha NTV amewafurahisha mashabiki baada ya kusitisha kuripoti kati moja ya ripoti alizokuwa akifanya moja kwa moja kutoka wadi ya Mukuru Kwa Njenga jijini Nairobi wakati wa uchaguzi wa udiwani ambao uliahirishwa sehemu hiyo.

Mohammed anaonekana akijikaza kuendelea na kuripoti huku nyuma yake umati wa watu ukiwa umemzingira huku kila moja akifanya juhudi ya kujipenyeza mbele ili kuonekana. Hilo linafanya Mohammed kupoteza utulivu wake na kukatisha ripoti yake na kuwafokea watu hao kwa kuteta kwamba wanamsukuma.

Katika video hiyo ambayo kituo hicho kilipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Leila alilazimika kukatisha ripoti hiyo kwa njia ya kitaaluma na kuwapokeza kijiti wanahabari wenza Mark Masai na Smriti Vidyarthi kuendelea na habari studioni.

Majibu yake yaliwafurahisha wawili hao wa studio na Smriti akacheka, "Leila, wewe kweli ni shujaa wangu usiku wa leo," huku Mark akiangua kicheko.

Visa vya watu kutatiza ripoti na matangazo ya moja kwa moja si jambo geni kwani mapema mwaka huu pia video ya mwanahabari mmoja akimfokea mtu aliyejiingiza mbele ya kamera kutaka kuonekana ilisambazwa mitandaoni huku watu wakichekesha na klipu hiyo.

illy Lusige alikuwa akiripoti moja kwa moja kutoka mkutano mmoja wa kisiasa kwenye kaunti ya Bungoma ambapo mtu mmoja aliyeonekana kujawa na furaha, pengine ya kupata nafasi ya kuonekana runingani katika nafasi muhali kama hiyo, alijaribu kudakia mbele ya mwandishi huyo wa habari, ila Lusige akamsukuma na kumfokea vikali.

“Baada ya kutembelea Busia katika mkutano wa Azimio la Umoja…” Lusige alikuwa ameanza kabla ya kitendo hicho kutokea.

View Comments