In Summary

•Kevin Sowax amedokeza mipango ya kufanya ziara nyingine nchini Tanzania hivi karibuni na kumchukua ili kuishi naye kabisa.

•"Upendo mmoja. @hamisamobetto Nakumiss mon amor!” Kevin alisema.

Kevin Sowax na Mpenzi wake Hamisa Mobetto
Image: INSTAGRAM// KEVIN SOWAX

Mpenzi wa Hamisa Mobetto, Kevin Sowax amedokeza mipango ya kufanya ziara nyingine nchini Tanzania hivi karibuni na kumchukua ili kuishi naye kabisa.

Siku ya Jumatano, Mfanyabiashara huyo wa Togo ambaye kwa sasa anaishi China alishiriki picha yake akiwa na Hamisa Mobetto wakipanda ndege na kwenye sehemu ya maelezo akaweka wazi mipango yake na mama huyo wa watoto wawili.

"@hamisamobetto ninakuja kukuchukua hivi karibuni," Sowax alisema kwenye Instagram.

Katika picha hiyo ya kumbukumbu aliyoshiriki, mfanyibiashara huyo alionekana akimshika mkono Hamisa huku wakiingia kwenye ndege ya kibinafsi. Wote wawili walikuwa wamevaa nguo nyeupe zinazofanana.

Sowax pia alishiriki picha nyingine ya  mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumz na kutumia nafasi hiyo kueleza jinsi anavyompeza.

"Upendo mmoja. @hamisamobetto Nakumiss mon amor!” alisema.

Haya yanajiri wiki kadhaa baada ya mfanyibiashara huyo wa Togo kufanya ziara yake ya kwanza nchini Tanzania ambapo alifahamu nyumbani kwa Hamisa Mobetto na kukutana na watu wake.

Kevin aliwasili nchini Tanzania mwishoni mwa mwezi Agosti na Hamisa alimkaribisha na maua kabla ya wawili hao kushiriki mazungumzo na wanahabari.

Katika mahojiano, Kevin alibainisha kuwa yupo Tanzania kwa ajili ya mpenzi wake Hamisa. Pia alifichua kwamba angekutana na watoto wa mwanamitindo huyo, Fantasy Majizzo na Dylan Abdul Naseeb kwa mara ya kwanza.

"Itakuwa mara ya kwanza kukutana nao na siwezi kusubiri. Huwa tunazungumza kupitia simu, kupitia video ya simu. Tutakutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza,” Kelvin alisema.

Kelvin alifichua kuwa yeye binafsi hana watoto lakini akadokeza kuwa anasubiri kwa hamu kupata watoto kadaa na Hamisa.

"Siwezi kusubiri," alisema.

Mtogo huyo aidha alifichua kuwa alikutana na Hamisa katika hafla ya faragha nchini China na akavutiwa naye mara moja.

Alisema ni matumaini yake kumuoa mama huyo wa watoto wawili na kuwa na familia naye katika siku za baadaye.

"Hatujui mpango wa Mungu ni nini lakini natamani twende kila mahali pamoja hadi mwisho," alisema.

Mapema mwezi huu, Hamisa alifichua kuwa mpenzi wake alirejea Uchina kwa sababu za kikazi siku kadhaa baada ya kuwasili Tanzania.

Mama  huyo wa watoto wawili zaidi alikiri kwamba hakuweza kutia chochote mdomoni kwa siku kadhaa baada ya Kevin kuondoka.

“Mpenzi wangu amesharudi nchini kwao. Yaani tangu asubuhi sijala. Kweli kabisa,”  Bi Hamisa Mobetto alisema.

Aliongeza, “Inabidi afanye kazi. Na mimi inabidi nifanye kazi. Tutakutana katikati.”

View Comments