In Summary

“Mume wangu hajiamini. Kwanza kabisa, anakuanga na haya, anaanza kuogopa, anapanic..,” Zari alisema kabla ya kumwita mumewe  ‘fala’.

“Usiongee vibaya kuhusu mume wako kwa mtu yeyote… Niheshimu nisipokuwepo. Hiyo ndiyo ninayouliza, " Shakib alisema.

Zari na mumewe Shakib katika eneo la burudani
Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Mume wa Zari Hassan, Shakib Cham Lutaaya amejibu baada ya mwanasosholaiti huyo wa Uganda mwenye umri wa miaka 42 kudaiwa kumzungumzia vibaya kwenye sauti ya simu iliyosambazwa mitandaoni.

Sauti ya mazungumzo ya simu imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii ambapo mwanamke anayeaminika kuwa Zari anasikika akizungumzia jinsi Shakib anavyokosa kujiamini na ambavyo hajui lolote.

Katika sauti hiyo, mama huyo wa watoto watano anasikika akimwagiza mtu aliye upande wa pili wa simu atoe maelezo ya kina kwa mumewe mwenye umri wa miaka 31 huku akieleza kuwa hajazunguka dunia sana na anahitaji taarifa za wazi kuhusu nini kinatarajiwa juu yake.

“Ebu mpe briefing, mpe briefing. The only international trip amewahi kufanya Dubai na Dubai they are not so strict at the airport. Hiyo ya UK, hata kama uko na kila kitu wanauliza. Unahitaji kumpa maelezo mafupi,” Zari alisikika akisema kwenye sauti hiyo kabla ya kutoa maelezo zaidi kwa lugha ya Kiganda.

Aliendelea, “Unajua Shakib anapanic. Ni insecure hivyo. Kuingia kwenye counter hivyo mtu kumuuliza maswali na kuanza kujibu, anapanic. Yeye mwenyewe hajiamini vile alivyo, hajiamini. Anaanza kusema vitu vyake.”

Mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumz alisikika akitoa maelekezo zaidi kwa mtu aliyekuwa akiongea naye kwa lugha ya Kiganda.

 “Mume wangu hajiamini. Kwanza kabisa, anakuanga na haya, anaanza kuogopa, anapanic..,” Zari alisema kabla ya kuendelea zaidi kumwita kijana huyo wa miaka 31 ‘fala’.

 “Kwa upole wake hapo ndio nampendea, yeye ni fala,” aliongeza.

Kwa kweli, sauti hiyo inaonekana kumfikia Shakib ambaye alijibu kwa njia isiyo ya moja kwa moja juu ya jinsi alivyosikitoshwa na matamshi ya mkewe.

“Usiongee vibaya kuhusu mume wako kwa mtu yeyote… Niheshimu nisipokuwepo. Hiyo ndiyo ninayouliza, " Shakib alisema kwenye mtandao wa Facebook .

Mfanyibiashara huyo mwenye umri wa miaka 31 pia alizungumza kuhusu jinsi kiburi kinaweza kumfanya mtu kupoteza kitu kizuri.

"Mapenzi yatakufanya uonekane mjinga. Lakini kiburi kinaweza kukufanya ukakosa kitu ambacho hutapata tena,” alisema Shakib.

Je, huu unaweza kuwa mwanzo wa masaibu katika familia ya Lutaaya, miezi miwili tu baada ya harusi yao? Naam, tunasubiri tu na kuona nini kitatokea baadaye.

View Comments