In Summary

•“Usimtag mke wangu au mumewe kwa sababu sitakua na Bahati ilikwa tu picha. Wale wa oh nice couple tafadhali msituharibie Boma,” Kabi alisema.

•Bahati alimtaka mume huyo wa Milly Wajesus aondoe mikono yake kutoka kwa mkewe na hata kutishia kuikata.

Image: INSTAGRAM// KABI WAJESUS

Mwimbaji Kelvin Kioko almaarufu Bahati alimtishia mwanavlogu Kabi Wajesus kwa utani baada ya kuonekana kwenye picha akiwa amemshika mke wake Diana Marua.

Kabi alikuwa ameposti picha kadhaa zinazomuonyesha akiinua mguu wa Diana na kuwaomba wanamitandao kutowa’tag wapenzi wao akidai ni picha tu.

Mwanavlogu huyo wa The Wajesus Family aliwataka zaidi watumiaji wa Instagram kutoharibu ndoa zao na maoni yaliyopendekeza uhusiano kati yao.

“Usimtag mke wangu au mumewe kwa sababu sitakua na Bahati ilikwa tu picha. Wale wa oh nice couple tafadhali msituharibie Boma,” Kabi aliandika.

Aliongeza, “Diana Marua, asante kwa kuja kusherehekea Taji Wajesus tunakupenda. Na tag mwalimu wa Hisabati.”

Katika jibu lake kwa chapisho hilo, Bahati alimtaka mume huyo wa Milly Wajesus aondoe mikono yake kutoka kwa mkewe na hata kutishia kuikata.

“Bro nitakukata mikono.. toa mikono hapo.” Bahati alisema.

Kabi alijibu, "Yeye ndiye aliinua mguu sasa ningewacha aanguke kweli?."

Diana kwa upande wake alibainisha kuwa anapenda picha hizo na akasema alifurahia sherehe ya kuzaliwa ya mtoto wa Taji, Kabi.

Tazama maoni kadhaa kwenye picha za Kabi kutoka kwa baadhi ya wanamitandao;

@rachaelnyambu: Mnataka Milly Wajesus akaongezewe maji sindio.

@shantelwanjiku60: Ujaacha kushika viuno na ulikatazwa na mamaz.

@feliciamokz: Opportunity comes once in a lifetime.

@wambui_ndirituofficial: this is adultery.

@muyu_ke: You look good together.

Familia ya Bahati ni marafiki na familia ya The Wajesus na wanne hao huonekana pamoja mara kwa mara hasa wakati wa hafla maalum. Hakuna uhusiano mbaya unaojulikana kati yao kwani wanashirikiana katika mambo mengi.

View Comments