In Summary

•Katika video, Samidoh  anasikika akimuimbia Nyamu wimbo wa injili wa Kikuyu huku wakiwa wamekaa kwenye kiti kimoja.

•Nyamu hakuweza kuficha furaha yake kubwa na alitabasamu wakati wote alipokuwa akirekodi tukio hilo la kupendeza. 

Karen Nyamu na Samidoh wafurahia muda pamoja.
Image: HISANI

Video ya wapenzi na wazazi wenza mashuhuri, Karen Nyamu na Samuel Muchoki almaarufu Samidoh wakifurahia wakati pamoja imekuwa ikisambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kuzua hisia mseto miongoni mwa Wakenya ambao wamekuwa wakifuatilia hadithi yao ya mapenzi kwa karibu.

Katika video hiyo, Samidoh ambaye ni mwimbaji maarufu wa nyimbo za Mugithi anaonekana na kusikika akimuimbia mama huyo wa watoto wake wawili wimbo wa injili wa Kikuyu huku wakiwa wamekaa kwenye kiti kimoja.

"Muiritu uyu, (Njeri) wuiguaga atia, wee utaigite murigo thii?

Njiguaga oo gugufuata wee utaigite murigo thii,

Njiguaga oo gugufuata tondu nduigite murigo thii,

Njiguaga oo njuke uhe,tondu nduigite murigo thii, " Samidoh aliimba huku akiwa amemlalia seneta huyo kwenye kifua.

Kumaanisha: "Msichana huyu (Njeri), huwa unajiskia vipi, kama bado hujaweka mzigo chini? Nahisi kukufuata kama bado hujaweka mzigo chini, huwa nahisi nikuje unipee kwa sababu hujaweka mzigo chini."

Wakati akimwimbia mzazi huyo mwenzake, Samidoh alionekana akimgusa kwenye kiuno na makalio kuashiria kile alichokuwa akiimba kuhusu.

Wakati huo, seneta Nyamu hakuweza kuficha furaha yake kubwa na alitabasamu wakati wote alipokuwa akirekodi tukio hilo la kupendeza. Nyamu hata alijiunga na staa huyo wa Mugithi katika kuimba wimbo huo.

Haya yanajiri takriban wiki mbili baada ya Nyamu kutumbuiza wageni na wimbo wa Samidoh wakati wa harusi ya Akothee.

Wakati wa harusi hiyo ya Aprili 10, seneta huyo alisimama kwenye jukwaa, akapewa kipaza sauti na kuimba  wimbo wa mzazi mwenzake Samidoh akimshirikisha Joyce Wamama, 'Wendo wi Cama' (Mapenzi ni matamu).

Wageni walifurahia kutumbuizwa na mama huyo wa watoto watatu huku Akothee na mumewe mpya wakicheza pamoja naye.

"Asante, asante sana," Karen alisema baada ya kutumbuiza.

Karen Nyamu na Samidoh wamekuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu na tayari wana watoto wawili pamoja. Mkewe Samidoh, Edday Nderitu hata hivyo amekuwa akipinga suala la mume wake kuwa na wake wengi.

Takriban miezi miwili iliyopita, Edday alimwandikia Samidoh ujumbe mrefu kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akimuonya kwamba hayuko tayari kamwe kulea watoto wao katika ndoa ya wake wengi. Hii ilikuwa baada ya mwimbaji huyo kuonekana na Nyamu licha ya seneta huyo awali kudai uhusiano wao umefika mwisho.

View Comments