In Summary

•Katika kikao na mamake kwenye chaneli yake ya YouTube,Vishy alifichua kwamba kuolewa na mwanamume wa kipato kidogo hakukuwa katika mipango yake.

•Katika chapisho mnamo siku ya akina baba,Vishy alifichua kwamba aliogopa wazo la kuolewa akimlaumu baba yake mzazi.

Pritty Vishy na mpenzi wake DJ Starvy Pritty Vishy/Instagram
Image: INSTAGRAM// PRITTY VISHY

Mtayarishaji wa maudhui na mshawishi wa kidijitali Pritty Vishy hivi majuzi alifunguka kuhusu tamaa yake ya kuvunja mzunguko wa umasikini katika familia yake.

Katika kikao na mamake kwenye chaneli yake ya YouTube,Vishy alifichua kwamba kuolewa na mwanamume wa kipato kidogo hakukuwa katika mipango yake.

"Sitaki kuhangaika kama mama yangu, kiukweli sitaki kufuata nyayo za mama yangu,nataka niepuke misukosuko aliyopitia. Lengo langu ni kuwa na mwanamume mwenye uwezo wa kifedha,hivyo nitaweza kuhudumia familia yetu kwa raha,"alieleza.

Alipoulizwa mchango wake kama mke,Vishy alisiitiza kwamba majukumu yake kama mke na mama yametosha,na hakuona haja ya kufanya zaidi.

Alionyesha waziwazi nia yake ya kuondoka ikiwa mwenzake atashindwa kumtunza yeye na watoto wao,akisisitiza kwamba hatahatarisha furaha yake.

"Sileti chochote mezani,lakini mimi kuwa mke wako na kukuzalia watoto inatosha.Ikiwa wewe si mtu ambaye unatoa kwa furaha na kwamba autanipa mimi na watoto wetu maisha ya furaha,basi mimi najitoa,"Pritty alisisitiza

Katika chapisho mnamo siku ya akina baba,Vishy alifichua kwamba aliogopa wazo la kuolewa akimlaumu baba yake mzazi.

Alifichua kwamba aliandamwa na kumbukumbu za kukulia katika familia ya dhulma,ambapo baba yake alimtesa mama yake.

"Siku ya akina baba inakukumbusha jinsi baba yako alivyokuwa akimpiga mama yako mbele yako,baadhi yetu tunogopa ndoa kwa sababu ya hii,"aliandika.

Hivi majuzi,Pritty Vishy alionyesha furaha ya kuungana na mama yake aliporejea nchini baada ya miaka mingi ambapo alikwenda kusaka chuma ughaibuni.

View Comments