In Summary

•Vishy alidokeza kwamba amezama kabisa ndani ya dimbwi la mahaba na mcheza santuri wa Kenya ambaye anaishi Marekani.

•Starvy alimtambulisha Vishy kama mpenzi wake kwenye ukurasa wake na akamshukuru kwa kukubali kufichua uhusiano wao.

Pritty Vishy na mpenzi wake DJ Starvy
Image: INSTAGRAM// PRITTY VISHY

Mtumbuizaji mashuhuri wa tiktok Purity Vishenwa almaarufu Pritty Vishy hayupo sokoni tena.

Siku ya Jumapili, mpenzi huyo wa zamani wa mwimbaji Stivo Simple Boy alidokeza kwamba amezama kabisa ndani ya dimbwi la mahaba na mcheza santuri wa Kenya ambaye anaishi Marekani.

Alichapisha picha za mcheza santuri huyo anayefahamika kwa jina DJ Starvy na kunukuu kwa maneno matamu kwake

"Ninapenda kila kitu kuhusu wewe. Unafanya kila kitu kizuri. Unajua unanifanya kichaa, sawa? Nakupenda babe @dj_starvy," alisema.

Starvy alijibu kwa kumhakikishia kipusa huyo mwenye umri wa miaka 21 kuhusu mapenzi yake makubwa kwake.

"Unajua nakupenda mama watoto," alisema.

Vishy aliendelea, "Nakupea watoto  8 mapacha ndani na kadhalika."

Kwenye Instastori, mpenzi huyo wa zamani wa Simple Boy aliendelea kukikiri jinsi mpenziwe mpya anavyomkosesha usingizi.

"Ni wangu wa pekee," alisema.

Starvy pia alimtambulisha Vishy kama mpenzi wake kwenye ukurasa wake na akamshukuru kwa kukubali kufichua uhusiano wao.

"Nimekuwa nikisubiri siku hii nionyeshe dunia kwamba ni wewe nataka kuwa nawe. Shukran kwa kukubali tutangaze hadharani kuhusu safari yetu ya mapenzi . Maisha bila wewe yatakuwa ya huzuni," Starvy alisema.

Mwezi uliopita,  Pritty Vishy alidokeza kwamba amerejea sokoni kwa mara nyingine baada ya kutemwa na mpenzi wake.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, kipusa huyo mwenye umri wa miaka 21 alichapisha ujumbe wa huzuni akihutubia mpenzi wake ambaye alivunja moyo wake hivi majuzi licha ya kumpa mahaba mazito.

Vishy alibainisha kuwa hata alichorwa tatoo ya mpenzi kutokana na upendo wake kwake lakini aliishia kumvunja moyo.

"Unampa mtu moyo wako na anacheza nao.. hadi unamchora tattoo lakini wapi," Pritty  Vishy alilalamika.

Mpenzi huyo wa zamani wa Stivo Simple Boy hata hivyo alidokeza kuwa yupo tayari kusonga mbele na maisha yake.

Vishy alitengana na Simple Boy mapema mwaka jana, miezi michache tu baada ya mahusiano yao kujulikana hadharani.

Wawili hao hata hivyo ilidaiwa hawakuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi kwani Stivo alidaiwa kutaka kusubiri ndoa kabla ya kushiriki tendo la ndoa na mtumbuizaji huyo mwenye umri wa miaka 21.

View Comments